Pata taarifa kuu

Wanadiplomasia kutoka Marekani na Urusi kukutana Julai 17

Wanadiplomasia kutoka Marekani na Urusi watakutana wiki ijayo kujadili madai ya Urusi kuingilia Uchaguzi wa mwaka uliopita na kumsaidia Donald Trump kuibuka mshindi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake Donald Trump wakati wa mkutano wao kando ya mkutano wa G20 Hamburg, Julai, 7, 2017.
Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake Donald Trump wakati wa mkutano wao kando ya mkutano wa G20 Hamburg, Julai, 7, 2017. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Mbali na madai hayo, wanadiplomasia hao wajadiliana pia kuhusu vikwazo vya kiuchumi ambavyo viliwekewa Urusi wakati wa utawala wa rais wa zamani Barack Obama.

Mzozo wa Syria na Ukraine ni suala ambalo pia litajadiliwa.

Hayo yanajiri wakati mtoto wa kiume wa rais wa Marekani Donald Trump, amesema kuwa hakumfahamisha babake kuhusu mkutano na wakili raia wa Urusi ambaye alisema kuwa angesaidia katika kampeni yake ya uchaguzi

Donald Trump junior alikiambia kituoa cha habari cha Fox News kuwa mkutano huo haukuhusu chochote.

Alitoa barua pepe zake zikionyesha kuwa alikaribisha ombi la kukutana na wakili, ambaye alikuwa na uhusiano na Urusi, ambaye alikuwa na ujumbe potovu kumhusu Hillary Clinton.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.