Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI

Trump na Putin wakutana, wajadiliana mambo mbalimbali

Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wamekutana kwa mara ya kwanza, pembezoni mwa mkutano wa G 20 nchini Ujerumani na kuzungumzia masuala mbalimbali.

Rais wa Marekani Donald Trump (Kulia)  akiwa na mwenzake wa Urusi  Vladimir Putin (Kushoto)
Rais wa Marekani Donald Trump (Kulia) akiwa na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin (Kushoto) REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amesema mazungumzo kati ya viongozi hao yalikwenda vizuri na walijadiliana maswala ya usalama, biashara na madai ya Urusi kuingilia Uchaguzi wa Marekani mwaka uliopita.

Naye Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema kuwa rais Trump amekubali maelezo ya rais Putin kuwa nchi yake haikuingilia Uchaguzi wa Marekani.

Wakati uo huo, mkutano wa siku mbili wa viongozi kutoka mataifa hayo ya G20, unamalizika leo mjini Hamburg.

Viongozi hao wameendelea kuzungumzia maswala mbalimbali ya kiuchumu, usalama, suala la wakimbizi na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mkutano huu umekuwa ukifanyika huku maelfu ya waandamanaji wakiandamana katika mji huo kupinga mkutano huo kwa kile wanachosema, hauna maaana yoyote.

Polisi wapatai 15,000 wameonekana kufanikiwa kudhibiti maandamano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.