Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-USHIRIKIANO

Trump na Putin kukutana katika mkutano wa G20

Donald Trump atakutana na Vladimir Putin ana kwa ana Ijumaa hii, Julai 7 katika mkutano wa nchi zilizostawi kiuchumi (G20). Masuala ya kutoafikiana kati ya nchi hizi mbili yatajadiliwa, ikiwa ni pamoja na lile la Syria, Ukraine na Urusi kuishikilia Crimea, lakini pia madai ya kuingilia katika uchaguzi wa Marekani na vyombo vya kijasusi vya Urusi.

Siku ya Alhamisi ,bwana Trump alitumia hotuba yake nchini Poland kutoa wito kwa Urusi kuwacha kuyumbisha Ukraine na mataifa mengine.
Siku ya Alhamisi ,bwana Trump alitumia hotuba yake nchini Poland kutoa wito kwa Urusi kuwacha kuyumbisha Ukraine na mataifa mengine. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

awili hao wamesema kwamba wanataka kuimarisha uhusiano wao ambao uliharibika katika mgogoro wa Syria na Ukraine mbali na madai ya Urusi kuingilia kati uchaguzi wa Marekani.

Marais hao wanatarajiwa kujadiliana sana kuhusu maswala ya Syria na Ukraine.

Siku ya Alhamisi ,bwana Trump alitumia hotuba yake nchini Poland kutoa wito kwa Urusi kuwacha kuyumbisha Ukraine na mataifa mengine.

Warsaw, ambako alizuru siku ya Alhamisi, Donald Trump alituma ujumbe unaopingana na Vladimir Poutine. Rais wa Marekani alikosoa jukumu la Moscow la kusambaratisha mataifa jirani, lakini alisem aana mashaka na taarifa kutoka CIA na FBI katika udukuzi wakati wa uchaguzi wa urais nchini Marekani. Wakati huo huo Waziri wake wa Mashauri ya Kigeni Rex Tillerson alisema Washington inataka kushirikiana na Moscow nchini Syria, licha ya kutofautiana hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.