Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-CNN

Trump aendelea kuonyesha ukosoaji wake dhidi ya kituo cha CNN

Rais wa Marekani anaendelea kukosolewa duniani, siku moja baada ya kuchapisha video katika mtandao wa Twitter ikimuonyesha akimpiga mtu aliye na nembo kichwani ya shirika la habari la CNN.

Donald Trump  mara kwa mara amevituhumiwa vyombo vya habari kutoa taarifa za uongo. Donald Trump hapa katika Ikulu ya White House mjini Washington Juni 28, 2017.
Donald Trump mara kwa mara amevituhumiwa vyombo vya habari kutoa taarifa za uongo. Donald Trump hapa katika Ikulu ya White House mjini Washington Juni 28, 2017. REUTERS/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Video hii inaonekana kuchapishwa katika mtandao wenye kumpendelea Trump mapema wiki hii.

Vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni pamoja na CNN vimemlaumu rais wa Marekani kwa kuzua uchochezi na ghasia dhidi ya vyombo vya habari.

Rais Trump amekuwa kwenye malumbano na kituo cha CNN ambaye anasem ani kituo kinachosambaza 'taarifa bandia'.

Video hii iliyofanyiwa ukarabati ni ile inayomuonyesha Trump wakati alihudhuria michezo ya mieleka ya WWE mwaka 2007, ambapo 'alimshambulia' mmiliki wa michezo hiyo Vince McMahon.

Hata hivyo afisa katika masuala ya usalama nchini Marekani Thomas Bosset, ambaye awali alisema video hiyo haionekani kuwa ni kitisho kwa waandishi wa habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.