Pata taarifa kuu
BRAZIL-UFISADI

Rais wa Brazil afunguliwa mashtaka ya ufisadi

Rais wa Brazil Michel Temer amefunguliwa mashtaka ya ufisadi kwa madai ya  kukubali rushwa ya Dola za Marekani 150,000.

Rais wa Brazil  Michel Temer
Rais wa Brazil Michel Temer REUTERS/Ueslei Marcelino
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imetangazwa na kiongozi Mkuu wa Mashtaka Rodrigo Janot.

Rais Temer anatuhumiwa kupokea rushwa hiyo kutoka kwa kampuni ya uuzaji wa nyama ya mbuzi.

Hata hivyo, rais Temer amekanusha madai hayo na kusema kuwa atajitetea kudhihirisha kuwa hahusiki.

Kesi hiyo imewasilishwa na kufunguliwa katika Mahakama ya Juu na sasa Majaji wanaweza kuamua kuipeleka katika Mahakama ya chini ili kuanza kusikilizwa.

Bunge nalo linatarajiwa kupiga kura, kuamua ikiwa afunguliwe mashtaka au la.

Rais Temer, aliingia madarakani mwaka uliopita baada ya kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa wakati huo Dilma Rousseff, ambaye pia alifunguliwa mashtaka ya ufisadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.