Pata taarifa kuu
MAREKANI-TABIA NCHI

Trump aindoa nchi yake kwenye mkataba wa Paris kuhusu hali ya hewa

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuondoa nchi yake katika mkataba wa Paris, ulioafikiwa mwaka 2015 katika kupambana na ongezeko la joto duniani.

Kwa mujibu wa Donald Trump, hapa katika Ikulu ya White House tarehe 1 Juni, mkataba wa Paris ni "hasara tupu kwa Marekani."
Kwa mujibu wa Donald Trump, hapa katika Ikulu ya White House tarehe 1 Juni, mkataba wa Paris ni "hasara tupu kwa Marekani." REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza siku ya Alhamisi kwamba nchi yake imejiondoa kwenye mkataba wa Paris uhusuo hali ya hewa katika kupambana na ongezeko la joto duniani. Katika kampeni zake za uchaguzi, Donald Trump aliahidi kufanya hivyo kwa minajili ya kulinda ajira za Marekani na kauli mbiu yake "Marekani kwanza."

Rais Donald trump alisema mkataba wa Paris unakiuka uhuru wa Marekani. Itakuwa mzigo mkubwa wa kifedha na kiuchumi na kuzuia wakazi Marekani kunufaika na mafanikio kutoka kwa rasilimali ya nishati nchini Marekani. amesema Donald Trump.

Trump amesema hatua hii itamsaidia kujadili uwekezekano wa kuafikiwa kwa mjadala mwingine ambao hautawaathiri wafanyabiashara na wafanyakazi wa Marekani.

Mwaka ulipouta wakati wa kampeni za urais, Trump aliahidi kuondoa nchi yake katika mkataba huu ili kusaidia kuimarisha sekta ya mafuta na viwanda vya makaa ya mawe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.