Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Trump asema Marekani na Israel hazitakubali Iran kutengeneza silaha za Nyuklia

media Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kulia akisikiliza hotuba ya rais wa Marekani Donald Trump Mei 22 2017 mjini Tel Aviv REUTERS/Jonathan Ernst

Rais wa Marekani Donald Trump anayezuru Israeli, amesema Iran isiruhusiwe kutengeneza silaha za Nyuklia.

Akizungumza mjini Jerusalam, rais Trump ameishtumu  Tehran pia kwa kuyasaidia makundi ya kigaidi kama Islamic State katika eneo ya Mashariki ya Kati.

“Iran isikubaliwe kutengeza na kuwa na silaha za nyuklia,” alisema Trump baada ya kukutana na rais Reuven Rivlin.

Awali akizungumza akiwa mjini Tel Aviv baada ya kuwasili nchini humo, kiongozi huyo alisisitiza kuwa Marekani itaendelea kushirikiana na Israel katika maswala mbalimbali hasa ya kiusalama.

Aidha, ameelezea umuhimu wa kufufua mazungumzo ya amani kati ya Israeli na Palestina.

“Ziara yangu ya kwanza nje ya nchi, nimekuja katika eneo hilo takatifu kuthibitisha uhusiano wetu wa Israel na Marekani,” amesema Trump.

“Tuna nafasi ya kipekee ya kuleta amani , usalama na udhabiti katika eneo hili na watu wake, lakini zaidi ya yote kushinda ugaidi,” aliongeza.

Siku ya Jumanne atakutana na kiongozi wa Mamlaka ya Palestina Mahmud Abbas.

Trump ambaye ametokea nchini Saudi Arabia, anatarajiwa pia kuzuru Vatican kuonana na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana