Pata taarifa kuu
MAREKANI-SAUDI ARABIA

Tuko pamoja katika vita dhidi ya ugaidi, Trump awaambia viongozi wa nchi za Kiarabu

Rais wa Marekani Donald Trump amewaambia viongozi wa nchi za kiarabu na viongozi wa Kiislamu kuwa, nchi yake itaendeleza ushirikiano wa karibu kupambana na ugaidi.

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump REUTERS/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza siku ya Jumapili mjini Riyadh nchini Saudi Arabia, rais Trump amesema Marekani itashirikiana kikamilifu na mataifa hayo na mengine duniani kufanikisha vita hivyo kwa kutoa msaada wa kifedha na silaha.

“Nimeleta ujumbe wa urafiki, tumaini na upendo,” alisema Trump.

"Sijaja hapa kuwafunza au kuwasomea, bali nimeleta ujumbe wa ushirikiano," aliongeza.

Trump ameyalaani makundi la kigaidi kama Islamic State na Hezbollah na kuonya kuwa siku zao za kuendelea kutishia usalama wa dunia na Mashariki ya Kati umefika mwisho.

Aidha, amewataka viongozi wa dini ya Kiislamu kuendelea kukemea vitendo vya ugaidi, huku akisema magaidi wanaabudu kifo na si Mungu.

“Magaidi hawamwabudu Mungu, wanaabudu kifo,”

Trump amewaambia viongozi hao pia kuwa ni jukumu lao la kuwandoa magaid hao katika nchi zao, huku akitoa wito kwa viongozi wa dini ya Kiislamu kuwaondoa katika maeneo ya kuabudu.

“Waondoeni katika nchi zenu, waondoeni kabisa, katika maeneo ya kuabudu na katika dunia hii,” alisema Trump.

Trump amesema njia pekee na ya uhakika ya kuyashinda makundi haya ni kwa mataifa ya kiarabu kufanya bidii kuhakikisha kuwa makundi hayo hayapati fedha zinazowasaidia kuendeleza harakati zao.

Kuhusu Syria, Trump amelaani mauaji yanayoendelea nchini humo na kusema rais Bashar Al Assad anaendelea kuwauwa raia  wake bila hatia, na kutaka  Jumuiya ya Kimataifa kuisaidia Syria.

Wakati uo huo, Mfalme Salman wa Saudi Arabia ameishutumu Iran kwa kuunga mkono makundi ya kijihadi  na kuendeleza ugaidi katika eneo la Mashariki ya Kati matamshi ambayo yaliungwa mkono na rais Trump na kutaka Iran kuendelea kutengwa kimataifa.

Baada ya ziara yake nchini Saudi Arabia, Trump amesema anatarajiwa kuzuru Israel, Palestina, Vatican na Misri hivi karibuni.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.