Pata taarifa kuu
MEXICO-USALAMA

Rais wa Mexico aahidi kuimarisha usalama wa waandishi wa habari

Rais wa Mexico Enrique Peña Nieto ameahidi kuimarisha na kupanua mifumo ya kuwalinda waandishi wa habari, na kupambana na uonevu, siku mbili baada ya mauaji ya Javier Valdez, mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP na maarufu kwa masuala ya madawa ya kulevya.

Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto asema yuko tayari kutetea haki ya waandishi wa habari na watetezi wa hali za binadam. .
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto asema yuko tayari kutetea haki ya waandishi wa habari na watetezi wa hali za binadam. . HO / PRESIDENCIA DE MEXICO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake ya kwanza kuhusu mauaji hayo siku ya jumatano, Enrique Peña Nieto alitangaza kuwa serikali itatoa "uwezo wa kutosha kwa kuwalinda waandishi wa habari na watetezi wa haki za binadamu."

Akizungumza baada ya shutuma za mashirika yasiyo ya kiserikali juu ya kutoaadhibu wahusika wa mauaji ya waandishi wa habari nchini Mexico, rais wa Mexico pia aliahidi kuimarisha ofisi maalum ya mashitaka iliyoundwa mwaka 2010 kuchunguza uhalifu na vitisho dhidi ya waandishi wa habari.

Vile vile, uchunguzi unaoendelea utaanzishwa upya, aliahidi Bw Peña Nieto. Kifo cha Javier Valdez, alieuawa kwa kupigwa risasi siku ya Jumatatu mchana, ni pamoja na mamia ya waandishi wa habari waliouawa nchini Mexico tangu mwaka 2000.

"Kitu ambacho watu wanatarajia, ni matokeo, yaani mapambano dhidi ya ukatili," alisema rais Peña Nieto, ambaye alisalia kimya kwa muda wa dakika moja kabla kutoa hotuba yake.

"Unyanyasaji dhidi ya waandishi wa habari na watetezi wa haki za binadamu umezidisha majeraha na majonzi katika jamii yetu," alisema Bw Peña Nieto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.