Pata taarifa kuu
MAREKANI

Mwanajeshi wa Marekani Chelsea Manning aachiliwa huru baada ya miaka 7 jela

Chelsea Manning, mwanajeshi wa Marekani aliyefungwa jela kwa makosa ya kuvujisha siri za serikali ya Marekami ameachiliwa huru.

Chelsea Manning picha aliyoipiga mwaka 2010
Chelsea Manning picha aliyoipiga mwaka 2010 Courtesy U.S. Army/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi Cynthia Smith amethibitisha kuachiliwa huru kwa Manning mwenye umri wa miaka 29, aliyekuwa amefungwa katika gereza la kijeshi la Fort Leavenworth, mjini Kansas.

Mwanajeshi huyo ambaye ana jinsia ya kike na kiume, alikuwa amehukumiwa gerezani kwa muda wa miaka 35 lakini ameondoka baada ya kutumikia kifungo cha miaka saba.

Kabla ya kuondoka kwake, rais wa zamani Barrack Obama aliagiza kupungiziwa kifungo na baadaye kuachiliwa huru.

Alikamatwa na kufunguliwa mashataka baada ya kupatikana na kosa la kutoa taarifa za siri kwa mtandao wa Wikileaks unaoongozwa na Julian Assange  kuhusu operesheni za kijeshi na maswala mengine ya kidiplomasia.

Miongoni mwa taarifa zilizovujishwa na Manning ni kuhusu operesheni za kijeshi nchini Afganistan na Iraq.

Akiwa jela, Manning alijaribu kujiua lakini pia kugomea chakula kinachotolewa na maafisa wa gereza hilo.

Mashirika ya kutetea haki za Binadamu kama Amnesty International na Wikileaks yamekuwa yakishutumu kufungwa kwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.