Pata taarifa kuu
MAREKANI

Ukosefu wa ajira wapungua mara 10 nchini Marekani

Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Marekani kimepungua kwa kiwango kikubwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 10 kufuatia kuimarisha ujenzi wa ajira mwezi April , hatua ambayo inampa ahueni rais Donald Trump baada ya kukabiliwa na takwimu mbaya za kiuchumi mapema katika urais wake.

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kushuka mwezi Machi, wakati ajira mpya zilishuka chini kutokana na dhoruba ya majira ya baridi, idara ya uchumi wa Marekani iliongeza ajira mpya zinazokadiriwa kufikia 211,000 huku kiwango cha ukosefu wa ajira kikishuka mara kumi hadi asilimia 4.4, kiwango ambacho ni cha chini zaidi tangu Mei 2007, wizara ya Kazi imearifu jana Ijumaa.

Ikulu ya White house imepongeza habari hizo baada ya robo ya kwanza wakati takwimu za uchumi zikionekana kuwekwa sawa na Rais Trump ameapa kuongeza ajira mpya milioni 25 katika kipindi cha mwongo mmoja jambo ambalo linakosolewa na wachumi kuwa halitawezekana.

Naibu msemaji wa ikulu Sarah Huckabee Sanders amesema idadi ya ajira inaonesha ajenda ya rais ya kupunguza kodi na kukuza uchumi wa Marekani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.