Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/09 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/09 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Republicans wapiga kura ya ndio kufuta bima ya afya ya Obamacare

media Rais wa Marekani Donald Trump akiwa na wabunge wa Republican katika Ikulu ya White House baada ya kupitishwa kwa mswada wa kutupilia mbali bima ya afya ya Obamacare REUTERS/Carlos Barria

Wabunge wa chama cha Republican nchini Marekani wamefanikiwa kupitisha mswada unaondoa na kubadilisha mpango wa  bima ya afya ya Obamacare iliyoanzishwa na rais wa zamani Barrack Obama.

Mswada huo ulipita baada ya wabunge wa Republican kufanikiwa kupata kura 217 dhidi ya 213, hatua ambayo inaonekana ni ushindi kwa rais Donald Trump ambaye kwa muda mrefu amekuwa akipinga bima hii.

Trump aliyekutana na viongozi wa Republican katika IKulu ya White House, amesema amefurahia sana mafanikio ya wabunge wake na kusisitiza kuwa bima ya Obamacare imekufa.

Kulikuwa na maandamano nje ya majengo ya bunge jijini Washington DC kupinga hatua ya wabunge wa Republican. Hakuna mbunge yeyote wa Democratic aliyeunga mkono mswada huo ambao sasa utapigiwa kura katika bunge la Senate.

Wanaisasa wa Democratic akiweno Hillary Clinton aliyewania urais mwaka uliopita, wamelaani hatua hiyo na kusema inaondoa matumaini ya Wamarekani wa kipato cha chini kupata haki ya kupata huduma ya afya.

Serikali ya Trump inatarajiwa kutumia Dola za Marekani Milioni 8, kuzindua mpango mpya wa bima ya afya, mpango ambao hata hivyo unakosolewa sana na watalaam wa afya na wanasiasa wa upinzani kuwa utawaacha raia wengi bila bima.
 

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana