Pata taarifa kuu
SYRIA-MAREKANI

Marekani yasema iko tayari kuishambulia tena Syria ikiwa itakiuka sheria za kimataifa

Marekani jana Ijumaa imeonya kuwa iko tayari kushambulia tena Syria baada ya kutekeleza shambulizi la kombora katika uwanja wa ndege wa kijeshi nchini humo,eneo ambalo linaaminiwa kuwa serikali ya Syria ilirushia silaha za kemikali kwenda katika mkoa wa Idlib wiki hii na kusababisha vifo vya watu 86 wakiwemo watoto 27 na kuwajeruhi wengine 500, hatua ambayo imechochea miito ya kukomesha vita ya miaka sita nchini humo.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley  akiwa na picha za waathirika wa shambulizi la kemikali nchini Syria wakati wa mkutano wa UNSC
Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley akiwa na picha za waathirika wa shambulizi la kemikali nchini Syria wakati wa mkutano wa UNSC Shannon Stapleton/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Balozi wa Marekani kwenye umoja wa Mataifa Nikki Haley ametoa onyo hilo katika kikao cha dharura cha Baraza la Usalamala umoja huo kilichoitishwa baada ya shambulizi la Marekani, ambalo lilitekelezwa kama adhabu dhidi ya serikali ya rais Bashar al-Assad.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.