Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI

Trump asema Marekani inaweza kukabiliana na Korea Kaskazini bila msaada wa China

Rais wa Marekani Donald Trump amesema nchi yake itakabiliana na tishio la Nyuklia kutoka Korea Kaskazini hata bila ya msaada wa China.

Mojawapo ya majaribio ya silaha za Nyuklia ya Korea Kaskazini
Mojawapo ya majaribio ya silaha za Nyuklia ya Korea Kaskazini ©KCNA
Matangazo ya kibiashara

Trump amesema ikiwa China haitashughulikia tishio hilo, Marekani itafanya hivyo.

Kiongozi huyo wa Marekani ameliambia Jarida la Marekani la Financial Times kuwa Marekani peke yake inaweza kukabiliana na tishio hili.

Trump ametoa matamshi haya wakati huu anapojiandaa kumkaribisha rais wa China Xi Jinping katika Ikulu ya Marekani wiki hii jijini Washington DC.

“China ina ushawishi mkubwa sana dhidi ya Korea Kaskazini. Wakitusaidia watakuwa wamejisaidia wenyewe lakini wasipofanya hivyo, halitakuwa jambo jema kwa yeyote,” alisema Trump.

Hata hivyo, Trump hajasema ni mbinu gani atatumia kukabiliana na tishio hili.

Kuna hofu kuwa huenda Korea Kaskazini ikatengeneza silaha za Nyuklia ambazo zinaweza kufika Marekani na kuleta madhara makubwa katika siku zijazo.

Pyongyang imekuwa ikijaribu silaha zake za masafa marefu na mafupi mara kwa mara na kuonesha kuwa ipo tayari kwa vita dhidi ya Marekani na maadui zake.

Hali hii imeendelea kuzua hali ya wasiwasi kwa mataifa jirani kama Japan na Korea Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.