Pata taarifa kuu
MAREKANI-CLIMATE

Annan: Dunia isivunjike moyo na uamuzi wa Trump kuhusu mabadiliko ya tabia nchi

Katibu mkuu wa zamani wa umoja wa Mataifa Kofi Annan, ametoa wito kwa dunia kuendelea na mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi licha ya uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump kutoa amri ya kuondolewa kwa sheria zilizokuwa zimetiwa saini na mtangulizi wake Barack Obama kuhusu taifa hilo kuwa na nishati salama.

Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan (katikati)
Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan (katikati) DR
Matangazo ya kibiashara

Annan amesema haya wakati akihutubia kwenye mkutano wa mwaka wa mfuko wake kuhusu kilimo jijini Brussels, ambapo amesisitiza kuwa makubaliano yaliyotiwa saini jijini Paris yaliweka nia nzuri ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Annan anasema Marekani inaweza kujitoa kwenye makubaliano hayo kutokana na sera za rais Trump au ikaamua kusitisha kwa muda utekelezaji wake..lakini dunia haipaswi kusimama kwa sababu Marekani imeamua kufanya yote haya.

Mshindi huyu wa zamani wa tuzo ya Nobel, amegusia pia kuhusu madhara ya mabadiliko ya tabia nchi na namna gani nchi zinaweza kuboresha mfumo wa chakula ili kulisha mamilioni ya watu duniani wanaokabiliwa na baa la njaa kutokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Reuters

Kofi Annan ameeleza umuhimu wa uhitaji wa kuwa na uwekezaji wa nguvu kwenye nchi zinazoendelea na mfumo wa chakula ambao utawezesha kuzalisha chakula kwa wingi kwa kutumia rasilimali chache.

Katibu mkuu huyo wa zamani ametoa wito kwa nchi duniani kuhakikisha zinawajibika na kutoa mchango wao katika kuhakikisha zinatekeleza na kufikia maendeleo endelevu kama yalivyoainishwa kwenye mkataba wa umoja wa Mataifa.

Matamshi ya Annan yamekuja ikiwa ni saa chache tu zimepita toka rais wa Marekani, Donald Trump atie saini amri ya kuondoa makataa iliyokuwa imewekwa na mtangulizi wake kwenye matumizi ya nishati ya makaa ya mawe, akisema sheria zilizokuwa zimewekwa zinawanyima raia wa Marekani ajira.

Wataalamu wa masuala ya mazingira wanaonya kuwa uamuzi wa rais Trump hautakuwa na madhara tu ndani ya Marekani lakini pia utakuwa na madhara kidunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.