Pata taarifa kuu
CIA-WIKILEAKS

WikiLeaks yavujisha nyaraka za siri za CIA yaonya aina mpya wanayotumia kudukua taarifa

Mtandao wa WikiLeaks umechapisha taarifa za siri ambazo imesema shirika la ujasusi la nchini Marekani, CIA, linauwezo wa kusikiliza maongezi ya wananchi kupitia njia ya televisheni, kutumia programu maalumu na hata kuna uwezekano wakaliongoza gari lako.

Watu wawili wakiwa na lap top mbele ya nembo maalumu ya shirika la ujasusi la Marekani, CIA
Watu wawili wakiwa na lap top mbele ya nembo maalumu ya shirika la ujasusi la Marekani, CIA REUTERS/Dado Ruvic
Matangazo ya kibiashara

Mtandao huo umechapisha zaidi ya nyaraka elfu 9 ambazo imesema zinatoka shirika la ujasusi la CIA, taarifa ambazo inasema ni nyingi zaidi kuwahi kuchapishwa kwa taarifa za siri za CIA.

WikiLeaks imedai kuwa nyaraka kadhaa za CIA, hasa vifaa walivyofanyia udukuzi inadhihirisha namna gani shirika hilo la ujasusi lina uwezo mkubwa wa kuiba taarifa za wananchi na kwamba wao pia walizipata kutoka mitandao mingine na kuchapisha sehemu tu ya taarifa walizonazo.

"Nyaraka hizi za kipekee, ambazo zinaainisha tarakimu za siri zaidi ya milioni, zinampa mmiliki wake kufanya udukuzi katika shirika la CIA," umeonya mtandao huo ambao umesema kuna hatari ya kutokea vita ya kimtandao.

Hata hivyo CIA wala ikulu ya Washington hazijasema chochote ikiwa taarifa zilizochapishwa zina ukweli wowote au halisi.

Katika kile kinachoonekana kulikuwa na ushirikiano mkubwa, kuvuja kwa taarifa hizi kutakuwa ni aibu nyingine kubwa kwa mashirika ya ujasusi ya Marekani, ikiongeza ile ilivyofanywa na jasusi Edward Snowden's mwaka 2013 ambaye alivujisha taarifa za siri za shirika hilo na pia kukamatwa kwa jasusi wa zamani akiwa na nyaraka nyingi za siri nyumbani kwake alizozichukua kwa zaidi ya miaka 20.

WikiLeaks inasema hivi sasa CIA inafanya udukuzi hata kwa idara ya usalama wa taifa ambayo ndio shirika kubwa la Serikali katika kufanya upelelezi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.