Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-UCHAWI

Vita ya Wachawi kumuondoa Trump mamlakani vyaanza

Usiku wa manane siku ya Ijumaa, Wamarekani wanaoamini uchawi nchini kote Marekani, waliandaa matambiko yenye nia ya kumuondoa Trump uongozini. Hadi sasa ukurasa wa Facebook wa matambiko hayo umepata wafuasi 10,500.

Rais wa Marekani Donald Trump na Mkewe Melanie Trump wakiwasili kanisani katika Kanisa Kuu la Taifa mjini Washington, Marekani, Januari 21, 2017.
Rais wa Marekani Donald Trump na Mkewe Melanie Trump wakiwasili kanisani katika Kanisa Kuu la Taifa mjini Washington, Marekani, Januari 21, 2017. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Hatua hizo zimezua ghadhabu kotoka kwa Wakirsto ambao wamewalaumu wachawi hao wa kutangaza vita vya kiroho.

Wachawi hao wanapanga kurudia tambuko hilo hadi pale Trump atakapoondoka ofisini. Tambiko lingine litafanyika machi 26.

Wapinzani wengi wa rais wa Marekani Donald Trump, wanaamini kuwa itawabidi wasubiri kwa miaka minne ili aweze kuondoka madarakani.

Hata hivyo wachawi nchini Marekani hawakubaliani na hilo na kubaini kwamba bw Trump anapaswa kuondoka mamlakani kabla ya muhala wake wa kwanza kumalizika.

Wakati huo huo chama cha Wakiristo kilitangaza tarehe 24 mwezi Februari kama siku ya maombi ya kuukabili uchawi huo.

Rais wa Marekani Donald Trump mpaka sasa hajazungumzia lolote kuhusu mkasa huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.