Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SIASA

Trump apuuzilia mbali kuwa na mawasiliano na Urusi

Rais wa Marekani Donald Trump amesisitiza kuwa sio yeye wala mtu kutoka kwenye kambi ya kampeni yake alikuwa na mawasiliano na maofisa wa juu wa Serikali ya Urusi kuhusu kuingilia uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Picha ya zamani: Vladimir Putin akiwa na Michael Flynn, mshauri wa zamani wa Usalama wa Taifa wa Donald Trump wakichangia chakula cha baaad ya maadhimisho ya miaka kumi ya runinga ya Urusi ya Russia Todaymwezi Desemba mwaka 2015.
Picha ya zamani: Vladimir Putin akiwa na Michael Flynn, mshauri wa zamani wa Usalama wa Taifa wa Donald Trump wakichangia chakula cha baaad ya maadhimisho ya miaka kumi ya runinga ya Urusi ya Russia Todaymwezi Desemba mwaka 2015. Mikhail Klimentyev/Kremlin/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Aidha, aliyekuwa mshauri wake wa masuala ya usalama aliyejiuzulu, huku akiendelea kutilia mkazo kuhusu sera yake ya kuzuia baadhi ya raia na wahamiaji kutoka kwenye mataifa 7 ya kiislamu duniani.

Trump ameendelea kuikosoa idara ya usalama wa taifa kwa kuvujisha taarifa hizo, ambazo nyingine amesema ni za uongo.

Hayo yakijiri askari wa zamani aliyekuwa amependekezwa na Rais wa Marekani Donald Trump kuwa mshauri wake wa masuala ya usalama wa taifa amekataa kazi hiyo.

Robert Harward alitarajiwa na wengi kuchukua wadhifa huo ulioachwa na Michael Flynn aliyefutwa kazi na Bw Trump Jumatatu wiki hii.

Afisa mmoja wa ikulu ya White House alisema sababu ya Bw Harward kukataa nafasi hizo ni kwamba ana majukumu mengi ya kifamilia na kifedha.

Pigo hilo kwa Bw Trump, la kukataliwa kwa uteuzi wake na Harward, lilitokea saa chache baada ya Bw Trump kupuuzilia mbali ripoti kwamba utawala wake umekumbwa na mtafaruku mkubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.