Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-VYOMBO VYA HABARI

Donald Trump avilaumu vyombo vya habari

Rais wa Marekani Donald Trump, anavilaumu vyombo vya Habari kwa kufanya kazi yake kuwa ngumu na kutoripoti mazuri ambayo serikali yake imefanya tangu alipochukua uongizi wa taifa hilo mwezi uliopita.

Trump amekuwa akikosolewa kutokana na uamuzi wake wa kuzuia kwa muda wageni kutoka mataifa saba ya Kiislamu kutembelea Marekani.
Trump amekuwa akikosolewa kutokana na uamuzi wake wa kuzuia kwa muda wageni kutoka mataifa saba ya Kiislamu kutembelea Marekani. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo, mwanajeshi Mstaafu Robert Harward, amekataa uteuzi wa rais Trump kuwa mshauri wake wa maswala ya usalama, akisema sababu za kifamilia na za kifeha hazimruhusu kuchukua nafasi hiyo.

Harward, kwa sababu za kifamailia na za kifedha zimemfanya kutokubali nafasi hiyo iliyokuwa inashikiliwa na Michael Flynn aliyejiuzulu wiki hii kwa madai ya kutoa taarifa za siri kwa Urusi.

Trump amekuwa akikosolewa kutokana na uamuzi wake wa kuzuia kwa muda wageni kutoka mataifa saba ya Kiislamu kutembelea Marekani, uamuzi ambao hata hivyo umezuiwa na Mahakama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.