Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-USAFIRI

Utawala wa Trump watetea marufuku dhidi ya wahamiaji

Idara inayoshughulikia maswala ya sheria na haki nchini Marekani inaitaka Mahakama ya rufaa nchini humo kuondoa pingamizi la kuzuia agizo lililotolewa na rais Donald Trump kuwazuia wahamiaji kutoka mataifa saba ya Kiislamu kuingia nchini humo.

Utawala wa Trump ulisema Jumatatu, Januari 6, 2017 kwamba agizo dhidi ya uhamiaji liko chini ya "mamlaka ya Rais" na kushutumu uamuzi wa jaji kuzuia utekelezaji wa agizo hilo.
Utawala wa Trump ulisema Jumatatu, Januari 6, 2017 kwamba agizo dhidi ya uhamiaji liko chini ya "mamlaka ya Rais" na kushutumu uamuzi wa jaji kuzuia utekelezaji wa agizo hilo. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Idara hiyo imekata rufaa kutaka zuio hilo kuondolewa kwa kile inachosema kuwa, rais Trump alifanya uamuzi huo kwa sababu za usalama wa taifa.

Akizungumza na wanajeshi, rais Trump amesema uamuzi wake ni kuzuia watu wabaya kuja Marekani.

Marufuku iliyowekwa na Mahakama ya rufaa imewapa afueni wakimbizi kutoka mataifa hayo ya Kiislamu na wameanza kwenda Marekani.

Wakati huo huo Mahakama ya Rufaa ya San Francisco inatazamiwa kutathmini kuhusu uhalali wa agizo la Donald Trump juu ya marufuku ya visa kwa wananchi kutoka nchi saba za Kiislamu. Utawala wa Marekani ulitoa Jumatatu, Januari 6 nyaraka zilizoombwa na majaji watatu ambao watachukua uamuzi utakaoleta madhara makubwa.

Mahakama ya Rufaa ya San Francisco imetangaza kuwa itashughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo. Mahakam hiyo imesema kuwa itawasikiliza Jumanne mchana wiki hii kambi inayounga mkono na ile inayopingaagizo la Donald Trump. Majaji watatu hawatasubiri uamuzi wao kwa muda mrefu. Pande zote mbili zimeendelea kuonyesha misimamo yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.