Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Watu wanne wauawa katika Msikiti wa Quebec

media Eneo la usalama limetengwa karibu na Kitucho cha Utamaduni cha Kiislam mjini Quebec, baada ya watu watano kuuawa kwa kupigwa risasi Jumapili jioni Januari 29. REUTERS/Mathieu Belanger

Watu wasiopungua wanne waliuawa Jumapili jioni, Januari 29, wakati wa ufyatulianaji risasi katika Kituo cha Utamaduni cha Kiislam Jijini Quebec (CCIQ), katika mkoa unaozungumza Kifaransa magharibi mwa Canada. Eneo la Usalama limetengwa. Wakati huo huo watuhumiwa wawili wamekamatwa kwa mujibu wa polisi.

Kiongozi Kituo hicho cha Utamaduni wa Kiislam, Mohamed Yanguiamesema ufyatulianaji risasiulitokea katika Kituo cha Utamaduni cha Kiislam katika kata ya Sainte-Foy, muda mfupi baada ya saa mbili usiku saa za Canada. Tukio hili lilitokea wakati wa sala ya jioni. Watu kadhaa walikuwa katika eneo hilo, eneo pia linalojulikana kama Msikiti Mkuu wa Quebec.

Vyombo vya habari vimearifu kwamba watu watano wameuawa na wengi wengi kujeruhiwa. idara ya polisi ya mji huo (SPVQ) imethibitisha kuwa kuna watu waliouawa lakini haikubainisha idadi. operesheni kubwa bado inaendelea.

"Hali imedhibitiwa, polisiimehakikisha kwenye akaunti yake ya Twitter, maeneo yote yanalindwa na watu wanaoishi eneo hilo wameondolewa. uchunguzi unaendelea. "

Mashahidi wameliambia shirika la habari la Reuters kuwa waliona washambuliaji watatu. Wawili walikamatwa, polisi imethibitisha kwenye televisheni ya taifa.

Meya wa mji wa Quebec Régis Labeaume ameelezea masikitiko yake kwenye ukurasa wake wa Facebook na kutoa wito kwa ajili ya umoja: "Tudumishe umoja wetu. Mshikamano ni jibu bora kwa janga hili lililogharimu maisha ya watu wasio kuwa na hatia. "

Waziri Mkuu wa jimbo la Québec, Philippe, Couillard ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter.

Naye Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau amelani mauaji hayo.

Radio Canada imekumbusha kwamba Kituo cha Utamaduni cha Kiislam cha mji wa Quebec (CCIQ) "kililengwa na mwaka jana na watu wenye chuki, wakati ambapo kichwa cha nguruwe kiliwekwa kwenye moja ya milango yake, na wakati huo ilikua katika mafungo ya mwezi mtukufu wa Ramadhan. Na nyaraka zinazopinga Waislam zilisambazwa katika maeneo mbalimbali katika Jiji la Quebec katika wiki iliyofuatia tukio hilo. "

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana