Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Marekani yaamua kujenga ukuta kati yake na Mexico

media Ukuta wa Nogales, uliojengwa kwa kukomesha uhamiaji haramu kati ya Marekani na Mexico. AFP / Mark Ralston

Rais wa Marekani Donald Trump amesaini amri ya Rais ya kujengwa kwa ukuta kati ya Marekani na Mexico. Hii ni moja ya ahadi zake kubwa aliyoiweka wakati wa kampeni za zake za uchaguzi mwaka 2016.

Akizungumza na kituo cha televisheni cha ABC Bw Trump amesema kazi ya kujenga ukuta huo itaanza ndani ya mwezi mmoja, na kusisitiza kuwa Mexico watatakiwa kulipia gharama ya ujenzi huo.

Akizungumza na wafanyakazi wanaohusika na usalama wa taifa, Donald Trump amesema ukuta huo utazuia wahamiaji haramu na wafanyabiashara wa dawa za kulevya, na kubaini kwamba siku zao zimekwisha wao kuishi na kufanya uharibifu.
Amesisitiza kauli yake ya kutaka Mexico kulipia ukuta huo, licha ya Mexico kukataa kufanya hivyo.

Siku tano baada ya kuchukua hatamu ya uongozi, rais Donald Trump alisaini siku ya Jumatano amri yrnye lengo la kuweka "salama mpaka wa kusini mwa Marekani kutokana na ujenzi wa haraka wa ukuta.

Rais wa Mexico Enrique Peña Nieto amelaani mara moja mradi huo na ameahidi kutetea wahamiaji wa Mexico. "Nasikitika na kulaani uamuzi wa Marekani kuendelea kujenga ukuta ambao miaka kadhaa, badala ya kutuunganisha, wanasababisha mgawanyiko kati yetu" amesema katika ujumbe mfupi wa video uliorushwa kwenye akaunti yake ya Twitter.

Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto kwa sasa anashinikizwa kufuta mkutano wake na Rais Trump unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo mjini Washngton, ikiwa kama ni kujibu uamuzi huo wa Marekani kujenga ukuta.

Meya wa mji wa Mexico City Miguel Espinosa amesema kujengwa kwa ukuta huo, Marekani itajitenga yenyewe sio tu na Mexico bali na Amerika ya kusini yote.

Rais Donald Trump amesema pia kupitia upya mbinu zinazotumiwa kuwahoji washukiwa wa ugaidi, na pia kufungua tena magereza ya siri yanayoendeshwa na Shirika la Kijasusi la nchi hiyo CIA nje ya Marekani.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana