Pata taarifa kuu
MAREKANI-VYOMBO VYA HABARI

Rais mteule wa Marekani akutana kwa mara ya kwanza na vyombo vya habari

Rais mteule wa Marekani Donald Trump atakayechukua hatamu ya uongozi wa nchi Januari 20 amekutana kwa mara yake ya kwanza Jumatano hii na waandishi wa habari tangu achaguliwe Novemba 8.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump wakati wa mkutano na vyombo vya habari, mjini New York, Januari 11, 2017.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump wakati wa mkutano na vyombo vya habari, mjini New York, Januari 11, 2017. REUTERS/Lucas Jackson
Matangazo ya kibiashara

Akionekana ni mwenye hasira dhidi ya vyombo vya habari, rais mteule wa Marekani amezungumzia masuala mbalimbali kama vile mahusiano yake na Urusi, kurejelea upya sera ya Obamacare, na mpango wake wa kujenga ukuta na Mexico.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump ameshutumu tangu mwanzo wa mkutano wake na waandishi wa habari, taarifa za uongo zilizosambazwa katika baadhi ya vyombo vya habari nchini Marekani kuhusu mahusiano yake na Urusi.

Mahusiano na Putin

Rais mteule wa Marekani pia amesema hakujua kama angeweza kuelewana na Putin lakini ana matumaini kuwa itakuwa hivyo. Bilionea huyo kutoka chama cha Republican anasema ni "jambo muhimu" kuona rais wa Urusi anakuwa upande wake. "Kama Putin anampenda Trump, ni vizuri, si tatizo lolote," amesema Bw Trump.

Trump aachana na kazi ya biashara

Rais mteule wa Marekani Donald Trump pia ametangaza kukata mahusiano na shughuli zake nyingi za kibiashara na kifedha kwa kuhamisha mali yake yote katika kampuni ya "Trust" inayosimamiwa na wanawe wawili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.