Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 06/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 06/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 06/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Wafungwa 56 wapoteza maisha nchini Brazil

media Moja ya ghasia mbaya kushuhudiwa katika magereza yenye msongamano mkubwa wa wafungwa nchini Brazil. Getty Images

Nchini Brazil wafungwa 56 wameuawa katika ghasia mbaya zilizozuka usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu hii Januari 2 katika gereza la mji wa Manaus. Tukio kama hilo liliwahi kutokea mwaka 1992 na kusababisha vifo vya wafungwa 111katika gereza la Carandiru.

Ghasia hizo zilizuka kati ya makundi hasimu ya wafungwa Jumapili usiku na ziliweza kudhibitwa siku ya Jumatatu asubuhi.

Hii ni moja ya ghasia mbaya kushuhudiwa katika magereza yenye msongamano mkubwa wa wafungwa nchini Brazil.

Idadi ya vifo 56 inaweza kuongezeka, kiongozi wa usalama wa jimbo la Amazonas amesema.

Miili ya watu iliyokatwakatwa ilitupwa juu ya ukuta wa gereza, gazeti moja nchini humo limearifu.

Mamlaka ya magereza imekua ikifanya zoezi la kuhesabu wafungwa ili kujua idadi ya wale ambao walitoroka.

Brazil imekua ikikosolewa na mashirika ya haki za binadamu kwa msongamano wa mfumo wake wa magereza.

Mwaka 1992, ghasia zilisababisha vifo vya wafungwa 111 katika gereza la Carandiru katika jimbo la Sao Paulo.

Wengi waliuawa na polisi wakati ilipokua ikijaribu kuchukua udhibiti wa gereza hilo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana