Pata taarifa kuu
MAREKANI-CUBA-CASTRO

Fidel Castro kuzikwa Desemba 4

Baada ya kifo cha Fidel Castro, mwanamapinduzi wa Cuba na kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Jumamosi Novemba 26, serikali ya Cuba imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku tisa kuanzia Jumamosi baada ya kutangazwa kifo chake. Na mazishi ya kiongozi huyo yatafanyika Desemba 4, 2016.

Fidel Castro, Mwanamapinduzi wa Cuba, hapa akiwa nchini Argentina, Julai 21, 2006.
Fidel Castro, Mwanamapinduzi wa Cuba, hapa akiwa nchini Argentina, Julai 21, 2006. REUTERS/Andres Stapff
Matangazo ya kibiashara

Fidel Castro alizaliwa Agost 13, 1926 ambapo aliwahi kuwa mwanasiasa wa Cuba, mwanamapinduzi wa Kuba, Waziri Mkuu wa Cuba kati ya mwaka 1959 hadi mwaka 1976 na alikuwa Rais wa Cuba huru kati ya mwaka 1976 na 2008.

Akiwa mwanasiasa wa Cuba Fidel Castro alikuwa akifuata misimamo mbalimbali ya siasa za ulimwenguni hasa ule wa Marxist na Lenini na baadaye msimamo wa kimapinduzi wa Cuba.

Fidel Casto aliweza kufanya kazi kama katibu wa kwanza wa chama cha Kimkomunisti cha Cuba kati ya mwaka 1961 na 2011. Chini ya utawala wake ambao ulikuwa wa chama kimoja, Castro aliweza kusimamia misimamo yake kimataifa.

Fidel Castro aliweza kuwa katibu mkuu wa umoja usiofungamana na upande wowote ule kati ya mwaka 1979 na 1983 na mwaka 2006 na 2008.

Fidel Castro alikuwa akiamini katika kufanya mapinduzi ya mtutu wa bunduki iwe kwa Latino Amerika, Asia na Afrika. “Kuhoji juu ya mapambano ya silaha kuwa ndiyo njia pekee ya ukombozi ninaweza kujibu kuwa ndani ya hoja hii taifa letu hatuna budi. Katika raia wengi wa Cuba na mataifa mengi ya latino Amerika, hakuna njia nyingine ya kujikomboa zaidi ya matumizi ya mtutu. Hii inaonekana kuyafaa ata kwa mataifa mengine ya Asia na Afrika, “ alisema Fidel Castro.

“Kila mara mabeberu wanatumia kila namna wakiyaunganisha majeshi yao kwa kila taifa kuzuia demokrasia ya mapinduzi. Wanawanyonga watu kwa vitanzi, vitanzi hivi vinaweza kukatwa kwa kutumia mapambano ya silaha tu. Wanamapinduzi hawatumii silaha kama njia sahihi ya kujikomboa bali, hii ni njia inayoeleweka kwa haraka na wakandamizaji,” aliongeza Fidel Castro.

"Kwa hiyo raia wana njia mbili kuvumilia ukandamizaji au kupambana na adui kwa silaha. Ifahamike wazi kuwa adui huyu ana nguvu za uchumi na kila kitu ata tekinolojia. Mapambano yanajumuisha kutumia kila kitu mlichonacho haswa matumizi ya rasimalia watu,” alisema Fidel Castro katika mahojiano na mojawapo ya vyombo vya habari akiwa msituni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.