Pata taarifa kuu
MAREKANI-CUBA-CASTRO

Cuba: Fidel Castro, mahusiano ya karibu na Afrika

Mwanapinduzi, Fidel Castro, ambaye alifariki Jumamosi 26 Novemba akiwa na umri wa miaka 90, alikuwa na uhusiano wa karibu na Afrika, hasa kupitia rafiki yake Ernesto Che Guevara. Na Cuba ni nchi ambayo Nelson Mandela alizuru katika ziara yake ya kwanza baada ya kuachiliwa kutoka gerezani.

"Madiba" akiwa bega kwa bega na Fidel Castro (kulia) akaribisha mchango wa Wacuba kwa Afrika, Julai 26, 1991, mjini Matanzas.
"Madiba" akiwa bega kwa bega na Fidel Castro (kulia) akaribisha mchango wa Wacuba kwa Afrika, Julai 26, 1991, mjini Matanzas. OMAR TORRES / AFP FILES / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mapema miaka ya 1960, Fidel Castro alitumia zera zake za kwa ushirikiano na nchi nyingi za bara la Afrika. Lengo lake kuu ilikua kuwazindua Waafrika ili waweze kujikomboa kutoka mikononi mwa ukoloni wa nchi zenye nguvu.

Baada ya hotuba yake katika Umoja wa Mataifa mwaka 1964, Ernesto Guevara, maarufu "Che", aliteuliwa kuwa balozi wa mapinduzi ya Cuba barani Afrika. Alitumwa katika nchi ya zamani ya Congo iliyokua chini ya ukoloni wa Ubelgiji na mamia ya wapiganaji ili kusaidia kundi la waasi la Simba. Ilikua lengo la Cuba ambayo ilikua na matumaini ya kuchochea vita vya msituni mashariki mwa Congo, kama vile vilivyomfikisha Castro madarakani miaka mitano kabla. Ushirikiano wa kijeshi wa Cuba pamoja na makundi ya wanaharakati waliokua wakipinga ukoloni katika nchi za Afrika ulisaidia, na kufanikisha kwa watetezi wa uhuru kutoka chama cha PAIGC kilichokua kikitetea uhuru nchini Guinea-Bissau na Cape Verde.

Angola na MPLA

Lakini ni pamoja na Angola ambapo Fidel Castro alionekana jasiri na mwenye nguvu. Mwaka 1965, askari na washauri wa kijeshi walisaidia kundi la ukombozi wa watu la MPLA, likiongozwa na Agostinho Neto. Mwaka 1975, Cuba ilituma washauri wa kijeshi kwa kundi la MPLA, ambalo lilichukua madaraka nchini Angola. Lakini Rais Neto mara moja alikabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe dhidi ya kundi la waasi la UNITA, ambalo lilikua likisaidiwa na Afrika Kusini. MPLA ilisaidiwa na Cuba na Urusi ya zamani. Wakati huo Cuba iliwatuma askari wake 50,000 nchini Angola. Msaada ambao ulipelekea MPLA kusalia mamlakani.

"Madiba" bega kwa bega na Fidel Castro

Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Hayati Tata Nelson Mandela Madiba alishirikiana bega kwa bega na Fidel Castro na kukaribisha "mchango mkubwa wa mwanamapinduzi wa Cuba kwa mapambano ya uhuru" na dhidi ya ubaguzi wa rangi. Tangu kuanguka kwa utawala wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994 nchini Afrika kusini, nchi hizo mbili ziliendelea kuimarisha mahusiano yao. Cuba ni nchi ambayo Nelson Mandela alizuru katika ziara yake ya kwanza baada ya kuachiliwa kutoka gerezani, ziara kwa Fidel Castro, mshirika wake na rafiki yake wa karibu. Mandela alimmshukuru Castro kwa msaada wake wakati wa miaka ya mapambano ya chini kwa chini kwa chama cha ANC (African National Congress).

Ushirikiano katika nyanja ya afya

Hatimaye, moja ya sababu zilizopelekea Cuba kuingia na kuanzisha ushirikiano na Afrika ni diplomasia yake ya matibabu. Huduma ya matibabu ya Cuba kimataifa ni jina la sera hii ambayo imeendelea hadi leo nchini Cuba kuwatuma madaktari wa wake katika bara la Afrika. Madaktari wa Cuba ni mashuhuri kwa ajili ya mafunzo yao bora.

Programu za ushirikiano zilisainiwa na nchi nyingi, na Cuba imekua kutuma matabibu kwa kipindi cha miaka miwili kwa ujumla. Inasemekana kuwa Cuba imekua ikiwatuma maelfu ya madaktari katika pembe nne za dunia na hasa barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.