Pata taarifa kuu
MAREKANI

Marekani: Jill Stein mgombea wa chama cha Green ataka kuhesabiwa upya kwa kura

Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Green nchini Marekani, Jill Stein, amezindua harakati za kutaka kuhesabiwa upya kwa kura katika majimbo matatu yaliyokuwa na utata, akipata uungwaji mkono mkubwa.

Jill Stein alieyekuwa mgombea wa chama cha Green katika uchaguzi wa nchini Marekani, ambaye ametaka kuhesabiwa upya kwa kura
Jill Stein alieyekuwa mgombea wa chama cha Green katika uchaguzi wa nchini Marekani, ambaye ametaka kuhesabiwa upya kwa kura DR
Matangazo ya kibiashara

Timu ya kampeni ya Stein imesema kuwa ilikuwa inahitaji kukusanya kiasi cha dola za Marekani milioni 2 hadi kufikia Ijumaa ya wiki hii ili kulipia zoezi la uhesabuji upya wa kura za urais.

Hata hivyo malengo ya timu yake ya kampeni yalifikiwa mapema zaidi kuliko alivyotarajia, ambapo asubuhi ya Alhamisi nchini Marekani walifanikiwa kupata kiasi hicho cha fedha na kutaka nyongeza zaidi hadi kufikia dola milioni 4.

Katika kipindi cha saa 48 na 72 zilizopita, taarifa kutoka kwa wataalamu wa mitandao na kompyuta wanasema wamepata habari mbaya baada ya kufanya uchunguzi wao na kubaini kuna uwezekano mkubwa kuwa masuala ya kiusalama yalikiukwa nchi nzima.

Stein pamoja na wengine wanataka kufanyike uhakiki wa kura na kurudiwa kuhesabiwa upya baada ya uchaguzi wa Novemba 8, hasa kwenye majimbo ya Michigan, Pennsylvania na Wisconsin.

Hatua hii imefikiwa baada ya wataalamu kumfahamisha aliyekuwa mgombea wa Democrats, Hillary Clinton kuwa, kuna uwezekano upigaji kura wa njia ya kompyuta uliingiliwa na maharamia wa kwenye mtandao.

Rais mteule Donald Trump, alishinda kwenye majimbo ya Pennsylvania na Wisconsin, majimbo ambayo yalimsaidia kwa kiasi kikubwa kushinda kinyang;anyiro cha uchaguzi wa mwaka huu ambapo alivuka idadi ya kura za kimajimbo 270 zilizokuwa zikihitajika.

Jimbo la Wisconsin hadi sasa halijatangaza matokeo rasmi huku ikionekana wagombea hao wakikaribiana kwa karibu zaidi, hata baada ya wiki mbili toka kumalizika kwa zoezi lenyewe la upigaji kura.

Wakati kushindwa kwenye majimbo hayo kulichangia pakubwa kwa Clinton kuanguka kwenye uchaguzi wa mwaka huu, ameendelea kuongoza kwa kura za jumla na sasa anakaribia kufikia milioni 2 zaidi ya Trump, huku shinikizo zaidi likiongezeka kutoka kwa watu wa Liberal wakitaka uhakiki wa kura ufanyike upya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.