Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHUMI

Trump asema Marekani itajiondoa katika mkataba wa kibiashara wa Pacific

Rais mteule wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa Marekani itajiondoa katika mkataba wa kibiashara wa mataifa ya Pacific TPP.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump
Rais mteule wa Marekani Donald Trump Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Mwezi Februari mwaka huu, mataifa 12 yaliingia katika mkataba wa kushirikiana kibiashara na kuondoa vikwazo vya kufanya biashara kwa lengo la kuimarisha uchumi kati yao.

Mataifa hayo yaliyoingia katika mkataba huo ni pamoja na Brunei, Chile, New Zealand, Singapore, Australia, Canada, Japan, Malaysia, Mexico,Peru, Marekani na Vietnam.

Pamoja na kuinua uchumi, mkataba huo unalenga kusaidia kuunda ajira, kuinua uzalishaji wa bidhaa mbalimbali viwandani, kuleta ushindani wa kibiashara, kuhimiza uongozi bora na kuhifadhi mazingira.

Trump amesisitiza kuwa siku yake ya kwanza Ofisini baada ya kuapishwa tarehe 20 mwezi Januari mwaka ujao, ataiondoa nchi yake kwa kile anachosema nchi yake hainufaiki kiuchumi katika mkataba huo.

Aidha, ameongeza kuwa serikali yake itafanya mazungumzo mapya kuhakikisha kuwa Marekani inakuwa ya kwanza katika kila jambo na kuwafanya raia wa nchi hiyo kuwa na furaha.

Hata hivyo, serikali ya Japan imekosoa kauli hiyo ya Trump na kusema mkataba huo utakosa mwelekeo bila ya kuwepo kwa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.