Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Xi Jinping na rais mteule wa Marekani Donald Trump wakubaliana kukutana

media Rais mteule wa Marekani, Donald Trump REUTERS/Jonathan Ernst/File Photo

Rais wa China Xi Jinping na rais mteule wa Marekani, Donald Trump, wamekubaliana wakati walipozungumza kwa njia ya simu kuwa, watakutana mapema zaidi, kuzungumzia uhusiano baina ya nchi hizo mbili, limesema shirika la uta

 

Imearifiwa kuwa, rais Xi amemuambia Trump, ambaye kwenye kampeni zake alikuwa akiishambulia nchi yake na kutishia kuwa angeweka vikwazo vya asilimia 45 kwa bidhaa zinazotoka China, kwamba nchi zao zinahitaji kuwa na ushirikiano mzuri wa kiuchumi.

Viongozi hao wawili wamekubaliana kuwa na mawasiliano ya karibu ili kujenga mazingira mazuri ya kufanya kazi pamoja, na kwamba watakutana kwenye tarehe za wali za utawala wake kubadilishana mawazo hasa kwenye mambo ambayo yana maslahi mapana kwa nchi hizo mbili.

Kabla ya uteuzi wake, Trump alienda mbali zaidi na matamshi yake, akisema taifa hilo lenye uchumi imara kwenye bara la Asia kuwa ni "adui" yake, na kuapa kusimama kidete kuhakikisha maslahi ya Marekani yanalindwa.

Rais mteule Trump aliongeza kuwa hana nia yoyote ya kujihusisha na makubaliano yaliyofikiwa kati ya raia Obama na nchi hiyo, na hata kutishia kufutilia mbali mkataba wa kibiashara wa Trans Pacific unaozinufaisha nchi nyingi za Asia, mkataba ambao Trump alisema unawakosesha ajira raia wake.

Matamshi yake pamoja na msimamo aliokuwa nao kuhusu China, bado umeacha maswali mengi kuhusu namna ambavyo Trump atahakikisha anakuwa na uhusiano mzuri na nchi ya China.

CCTV kwenye taarifa yake imesema kuwa, rais Mteule Trump, ameonesha utayari wake wa kufanya kazi kwa karibu na rais Xi, na hata kudai kuwa ushirikiano wao wa Sino-US unaweza kutengenezewa mazingira mazuri zaidi ili kuzinufaisha nchi zao.

Kituo hicho cha taifa kimemuelezea rais mteule Trump, kama mtu ambayo ni mfano bora kwa diplomasia ya Uchina.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana