Pata taarifa kuu
UN-ANTONIO GUTERRES

UN: Antonio Guterres ateuliwa rasmi kuwa Katibu Mkuu

Antonio Guterres, kutoka Ureno atachukua mamlaka ya uongozi Januari 1 akimrithi raia wa Korea Kusini Ban Ki-moon kwenye wadhifa wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kwa lengo la kuimarisha taasisi hii dhaifu kutokana na mvutano kati ya mataifa yenye nguvu na kuenea kwa migogoro duniani.

Antonio Guterres, Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa.
Antonio Guterres, Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa. ONU
Matangazo ya kibiashara

Kamishna Mkuu wa zamani wa shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi, ambaye atakabialiana na mgogoro mkubwa tangu Vita Kuu vya Dunia, ameteuliwa rasmi Alhamisi hii na nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa muhula wa miaka mitano, baada ya kupokea Alhamisi iliyopita baraka kutoka nchi 15 wanachama wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Uteuzi wa Waziri Mkuu wa zamani wa Ureno, Waziri Mkuu wa zamani wa kwanza kushikilia nafasi hii, umekaribishwa kwa vifijo na nderemo.

"Karibu kwenye wadhifa usiyowezekana duniani", balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power amempongeza.

Bw Guterres amezitolea wito nchi zenye nguvu duniani kwenda mbali ya tofauti zao kuhusu Syria, wakati yakikaribia mazungumzo mapya ya kimataifa kuhusu mgogoro wa Syria ambao umewaua watu zaidi ya 300,000 na kusababisha maefu ya raia wa Syria kukimbilia nje ya nchi tangu mwaka 2001.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.