Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Wananchi wa Colombia wapinga makubaliano ya amani na FARC

media Kambi inayotetea makubaliano ya amani na AFRC yakata tamaa, baada ya matokeo ya kura ya maoni, Oktoba 2, 2016 mjini Bogota. REUTERS/John Vizcaino

Baada ya kura ya maoni , matokeo yanaonyesha kuwa wananchi wa Colombia wamepinga makubaliano ya amani na kundi la waasi la FARC, makubaliano yaliyoafikiwa hivi karibuni kati ya serikali na kundi hili la waasi.

Kwa mujibu wa matokeo rasmi ya kura ya maoni, kura ya "hapana" imeshinda kwa 50.21% dhidi ya 49.78% kwa kura ya "ndiyo."

Zaidi ya watu milioni kumi na tatu wamepiga kura, lakini wanaopinga makubaliano hayo wameshinda kwa kura zisizozidi elfu sitini.

Wakazi wa miji mbalimbali ndio wameonekana kupinga makubaliano haya kwa kiasi kikubwa. Katika mji wa Medellin, kwa mfano, kura ya "hapana" imeshinda kwa zaidi ya 60%. Magari yalizunguka kila sehemu yakiliza mahoni, huku raia wakifurahia ushindi katika mji mkuu huo wa jimbo la Antioquia, ngome kuu ya rais wa zamani Alvaro Uribe ambaye ambaye aliwataka wakazi wa jimbo hilo kupiga kura ya "hapana."

Ushindi huu ni pigo kubwa kwa upande wa kambi ya wale wanaotaka amani na wengi baadhi yao wamekata tamaa.

Matokeo haya yanaonyesha jinsi gani wananchi wa Colombia hawana imani na kundi la waasi la FARC. Wengi wao hawakukubali baadhi ya vipengele vya mikataba ya amani, hasa kile cha ushiriki wa kisiasa kwa waasi wa zamani na kile cha mahakama ya nchi inayoondokana na vita.
Rais Juan Manuel Santos ambae ametia saini makubaliano hayo wiki iliyopita katika sherehe zilizofana na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo kiongozi wa FARC, amesema hatojiuzulu.

Ameongeza kusema, makubaliano hayo ya amani ambayo yatamaliza mgogoro wa miongo mitano bado yanafanya kazi na kwamba yeye atasimamia amani hadi siku yake ya mwisho ofisini.

Jumapili hii Oktoba 2, kundi la waasi la FARC kupitia sauti ya kiongozi wake, lilielezea "masikitiko yake" kuona makubaliano haya yanapingwa na wananchi wa Colombia, huku likibaini kwamba halitoanzisha upya vita vya maguguni.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana