Pata taarifa kuu
MAREKANI-Hillary Clinton-DONALD TRUMP

Clinton amtuhumu Trump kwa kukiuka za sheria Marekani

Mgombea urais nchini Marekani kupitia chama cha Democratic Bi.Hillary Clinton, anasema mpinzani wake Donald Trump alivunja sheria za Marekani na kufanya biashara na nchi ya Cuba, licha ya vikwazo vya Marekani.

Wagombea wa rais Marekani Trump na Clinton wakati wa mjadala mkubwa kwenye televisheni Septemba 26, 2016.
Wagombea wa rais Marekani Trump na Clinton wakati wa mjadala mkubwa kwenye televisheni Septemba 26, 2016. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kampuni ya Trump kwa kisiri, ilishiriki biashara na Cuba kinyume na hivyo kuvunja marufuku iliyokuwa imewekwa na Marekani.

Inadaiwa kuwa kampuni ya Trump ilitumia zaidi ya Dola 68 za Marekani katika biashara hiyo mwaka 1998.

Hata hivyo, Trump kupitia kwa msemaji wake amesema fedha hazikulipwa na alikataa kuhusika katika biashara hiyo.

Trump katika kampeni zake kuelekea Uchaguzi mkuu mwezi Novemba amekuwa akisisitiza kuwa alikataa kuingia katika mikataba ya kufanya biashara nchini Cuba.

Clinton amemshtumu Trump kama mtu anayeweka maslahi mbele na kutofuata sheria za nchi ili kujinufaisha mwenyewe.

Ripoti hii inatarajiwa kuzua mjadala na majibizano makali kati ya Clinton na Trump katika siku zijazo kuelekea Uchaguzi mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.