Pata taarifa kuu
MAREKANI-USALAMA

Mtuhumiwa wa mashambulizi ya New York na New Jersey akamatwa

Hali ya wasiwasi ilikua bado ikiongezeka Jumatatu hii Septemba 19 mjini New Yor, nchini Marekani. Mtuhumiwa wa mashambulizi ya bomu Jumamosi juma lililopita katika mji wa Manhattan na New Jersey amekamatwa baada ya kurushiana risasi na polisi, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Marekani. Inaarifiwa kuwa alijeruhiwa wakati wa kukamatwa kwake.

Maafisa wa polisi katika eneo la Elizabeth, katika Jimbo la New Jersey, ambapo kilipuzi kimegunduliwa katika kituo cha treni.
Maafisa wa polisi katika eneo la Elizabeth, katika Jimbo la New Jersey, ambapo kilipuzi kimegunduliwa katika kituo cha treni. REUTERS/Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

Mtu mwenye uhusiano na mashambulizi ya New York amekamatwa na polisi, runinga za Marekani za NBC na CNN zimetangaza. Mtu huyo anajulikana kwa jina la Rahami Ahmad Khan, Mmarekani mwenye asili ya Afghanista, mwenye umri wa miaka 28 ambaye inadhaniwa kuwa anaishi, kwa mujibu wa tathmini za mwanzo, katika eneo la Elizabeth, mjini New Jersey. Hapo ndipo ambapo polisi ilimkamata Jumatatu hii, baada ya kurushiana risasi wakati ambapo alijeruhiwa.

Ni katika mji huo ambapo kumegunduliwa Jumatatu hii asubuhi mfuko wenye vilipuzi kadhaa. Wapita njia wawili ambao wamepatwa uoga kutokana na waya pamoja na bomba lililojitokeza nje ya mfuko uliotelekezwa nje ya kituo cha treni, walitoa tahadhari kwa polisi. Maafisa wa kutegua mabomu walikuaja haraka katika eneo la tukio.

Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post, msako unaendelea katika eneo la Elizabeth, ambapo inaishi familia ya mtuhumiwa.

Mkuu wa jimbo la New York, Andrew Cuomo, ameamua kuongeza idadi ya vikosi vya usalama katika mji wa New York. Askari polisi 1,000 wa ziada wametumwa katika mji huo Jumatatu hii ambapo mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa unaanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.