Pata taarifa kuu
MEXICO-USALAMA

Askari polisi 4 wauawa Mexico

Askari polisi wanne na rubani mmoja waliuawa nchini Mexico,baada ya helikopta waliyokuwemo kudunguliwa na genge la wahalifu. Shambulio jingine kama hilo lilitokea mwaka 2015, serikali ya Mexico imethibitisha tukio hilo, na imebaini kwamba vikosi vya usalama vinaendelea kuwasaka wahalifu hao.

Makabiliano kati ya gende la Jalisco linalojihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya na polisi hutokea mara kwa mara Mexico.
Makabiliano kati ya gende la Jalisco linalojihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya na polisi hutokea mara kwa mara Mexico. AFP
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lilizua mvutano kati yaviongozi Jumanne wiki, Gavana wa Jimbo la Michoacan (magharibi) alisemakwamba kwamba helikopta hiyo ilidunguliwa na genge la wahalifu kabla ya kurejea kauli yake.

Shambulizi la helikoptahiyo lilitokea katika mkoa wa Tierra Caliente, katika Jimbola Michoacan, ambapo biashara haramu ya madawa ya kulevya imekua sugu.

Katika ripoti ya awali, serikali ilisema kwamba watu wane kwa jumla ndio walipoteza maisha katika ajali hiyo, ikibaini kwamba askari polisi mmoja aliyekuwemo katika helikopta hiyo alinusurika. Lakini afisa wa mashtaka katika jimbo la Michoacan alithibitisha Jumatano vifo vya askari polisi wanne.

"Ndiyo, helikopta hiyo ilidunguliwa ," Kamishana wa usalama wa taifa alithibitisha Jumatano kwenye Radio Formula, akiongeza kuwa serikali ya Mexico inashirikiana naviongozi wa jimbo la Michoacan katika shughuli ya "kutafuta wahusika wa shambulio hilo."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.