Pata taarifa kuu
MAREKANI-UTURUKI

Uturuki: Obama na Erdogan kukutana Jumapili nchini China

Washington imetangaza mkutano kati ya Marais wa Marekani Barack Obama na Uturuki Recep Tayyip Erdogan nchini China, wakati ambapo serikali ya Uturuki ikiendelea na mashambulizi yake nchini Syria dhidi ya kundi la Islamic State na dhidi ya Wakurdi wanaoungwa mkono na Marekani.

RAis wa Marekani anatazamiwa kukutana na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan nchini China Jumapili hii Septemba 4, 2016..
RAis wa Marekani anatazamiwa kukutana na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan nchini China Jumapili hii Septemba 4, 2016.. Reuters / Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo, uliotangazwa Jumatatu wiki hii, utakaofanyika kando ya mkutano wa kilele wa viongozi kutoka nchi 20 utakuwa wa kwanza kati ya marais hawa wawili tangu mapinduzi ya Julai 15 yaliyoshindwa nchini Uturuki. Mapinduzi ambayo yamezua hali ya sintofahamu kati ya nchi hzi mbili. Uturuki unaomba kurejeshwa nyumbani Imam wa zamani Fethullah Gulen, anaishi uhamishoni nchini Marekani na ambaye anatuhumiwa kuongoza jaribio la mapinduzi nchini Uturuki.

Hali ya sintofahamu kati ya nchi hizi mbili iliongezeka kufuatia operesheni ya vikosi vya Uturuki iliyozinduliwa Jumatano dhidi ya wapiganaji wa kundi la PKK na wale wa kundi la YPG pamoja na wanajihadi wa kundi la Islamic State nchini Syria, nchi inayoendelea kukumbwa na mgogoro tata ambao umesababisha watu zaidi ya 290,000 kupoteza maisha tangu mwaka 2011.

Rais Erdogan alithibitisha Jumatatu katika taarifa yake kuwa mashambulizi yataendelea mpaka "mwisho wa tishio la makundi ya IS, PKK na YPG".

Ndege za kivita za Uturuki ziliendesha mashambulizi ya anga Jumatatu wiki hii dhidi ya ngome za kundi la wapiganaji wa PKK kaskazini mwa Iraq, katika mkoa wa Gara, Shirika la habari la Anadolu linalounga mkono serikali ya Uturuki limearifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.