Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAN

Je Marekani ililipa fidia ya Dola milioni 400 kwa Iran?

Gazeti la Wall Street Journal liliarifu Jumatano Agosti 3 kwamba Dola milioni 400 zilitumwa na Marekani kwa Iran katika mfumo wa fedha, kwa euro na faranga za Uswisi.

Utawala wa Barack Obama watuhumiwa kulipa fidia kwa Iran.
Utawala wa Barack Obama watuhumiwa kulipa fidia kwa Iran. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Gazeti hili la kila siku linasema kwamba fedha hizo, zilizohifadhiwa kwenyevifaa maalumu na kusafirishwa kwa ndege zilitumika kwa kulipa fidia kwa ajili ya kuachiliwa huru kwa Wamarekani watano. Washington imekanusha haraka taarifa hito huku ikithibitisha kutolewa kwa kitita hicho.

"Haikuwa fidia," amebaini Msemaji wa Wizara ya Fedha ya Marekani Mark Toner. "Kulipa fidia kwa ajili ya kuwakomboa mateka ni kinyume na sera za Marekani," amesisitiza msemaji wa White House Josh Earnest.

Kititia hiki cha Dola milioni 400 kinaendana sambamba na ulipaji wa deni la Marekani la kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979. Marekani na Iran zilisitisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1980. Fedha zililipwa mwezi Januari 2016 baada kushindwa kwa makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na baada ya kubadilishana wafungwa kati ya nchi hizo mbili: Raia wanne wa Iran wenyeuraia wa Marekani na mwandishi wa shirika la habari la Washington Post dhidiya msamaha uliotolewa kwa Wairan saba walikua wakizuiliwa.

Chama cha Republican, ambacho kinapinga makubaliano yaliyoafikiwa na utawala wa Obama, haraka sana kimeshikilia mikononi madai ya gazeti la kila siku la Wall Street Journal.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.