Pata taarifa kuu
MAREKANI-COLOMBIA

Marekani yasihi kundi la waasi la FARC

Kama waasi wa kundi la FARC nchini Colombia watakubali kusaini mkataba wa kudumu wa amani na serikali ya Bogota, Marekani iko tayari kuanzisha utaratibu wa kufuta kundi hilo kwenye orodha ya "makundi ya kigeni ya kigaidi," Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, alisema Jumatatu Agosti 1.

Ujumbe wa serikali ya Colombia na ule wa waasi wa FARC wakisaini mkataba wa usitishwaji mapigano..
Ujumbe wa serikali ya Colombia na ule wa waasi wa FARC wakisaini mkataba wa usitishwaji mapigano.. REUTERS/Stringer FOR EDITORIAL USE ONLY
Matangazo ya kibiashara

"Tunachunguza majina ya makundi ya kigaidi kwa nchi yoyote," amesema Kerry katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Colombia Maria Angela Holguin.

"Kama FARCitatia saini kwenye mkataba wa kudumu wa amani na kuheshimu makubaliano, kuweka chini silaha, kuzingatia mchakato wa amani na kukomesha machafuko, bila shaka Marekani haitosita kufuta kundi hilo kwenye orodha yake nyeusi ya makundi ya kigaidi. "

Kundi la waasi la FARC ililiwekwa tangu mwaka 1997 kwenye orodha ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ya "makundi ya kigeni ya kigaidi" ambayo yanakabiliwa na vikwazo vya kiuchumi na kisheria vya Marekani. FARC ni miongoni mwa makundi mengine kadhaa kama vile kundi la Islamic State, al-Qaeda, Hamas, Hezbollah, PKK na makundi mengine ya wanamgambo wa Kiislamu Mashirika mwa Asia, ambayo yamewekwa kwenye orodha ya makundi ya kigaidi na Marekani.

Kundi la FARC,ambalo lilisitisha mapigano tangu mwaka mmoja uliyopita, na serikali ya Colombia walisaini Juni 23, makubaliano ya usitishwaji moja kwa moja wa mapigano, kukomesha uhasama na kupokonya silaha waasi, ambavyo vitatekelezwa baada ya amani kupatikana.

Mkataba uliyosainiwa katika mji wa Havana, ambapo mazungumzo yalianza mwaka 2012, unaeleza kuwa baada ya mkataba wa amani kusainiwa, waasi watakusanywa katika maeneo 23 nchini Colombia chini ya udhibiti wa Umoja wa Mataifa, ambao utakua na jukumu la kukusanya na kuharibu silaha zao.

Kundi la waasi la FARC, ambalo lilianzishwa mwaka 1964 lina wapiganaji 7,000, kwa mujibu wa takwimu za serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.