Pata taarifa kuu
MAREKANI-BARACK OBAMA

Marekani: Dallas, Barack Obama atoa wito kwa maridhiano

Barack Obama alikuwa katika mji wa Dallas Jumanne, Julai 12, kuhutubia katika sherehe kwa heshima ya askari polisi watano waliouawa katika mji huo juma lililopita. Marekani imeendelea kukumbwa na visa vya mauaji ya watu weusi yanayofanyawa na askari polisi wasio na nidhamu.

Rais Barack Obama na mkewe kati ya Rais George W. Bush (kushoto) na Meya Mike Rawlings (kulia) katika sherehe kwa heshima ya askari polisi waliouawa.
Rais Barack Obama na mkewe kati ya Rais George W. Bush (kushoto) na Meya Mike Rawlings (kulia) katika sherehe kwa heshima ya askari polisi waliouawa. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Maandamano ya hapa na pale yamekua yakishuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo pamoja na mauaji ya maafisa wa polisi. Rais Barack Obama amebaini kwamba Marekani haigawanyiki kama wanavyosema baadhi ya wanasiasa.

Obama na mkewe pamoja na Bush na mkewe wameshikana mikono na kuonyesha ishara za urafiki na faraja, picha ambayo si ya kawaida. Ilikuwa Jumanne hii katika mji wa Dallas wakati wa sherehe kwa heshima ya askari polisi waliouawa wakati wa maandamano Alhamisi juma lililopita.

Barack Obama, alitoa hotuba ambayo waangalizi wa mambo wamesema ilikua muhimu. Lakini rais mwenyewe, baada ya sherehe10 za kufanana tangu mwanzo wa mamlaka yake, alionyesha kuchoka kwake.

"Mara nyingi nimekua nikihutubia katika sherehe kama hizi tangu nilipochaguliwa. Niliona jinsi gani muungano takatifu unaweza kutokomea haraka, ukizidiwa na kuanza kwa kesi za kawaida. Niliona kutokufaa kwa maneno kwa kuhamasisha mabadiliko ya kweli. Niliona jinsi gani maneno yangu yalikuwa haitoshi ... "

Barack Obama alimuweka kila mtu mbele ya majukumu yake. Askari polisi ambao hujihusisha katika vurugu au ubaguzi wa rangi, waandamanaji wanaotaka mapambano, na viongozi waliochaguliwa ambao wanapendelea kuepuka matatizo magumu yanayotakiwa kusimamiwa, kama mzunguko wa silaha.

"Askari polisi wanastahili heshima yetu na si dharau yetu"

"Tunajua kwamba idadi kubwa ya askari polisi wanafanya kazi ngumu na ya hatari pamoja na vyombo vya sheria. Wanastahili heshima yetu na si dharau yetu. Tunajua pia kwamba karne ya ubaguzi haikufutwa na kutiwa saini kwa sheria dhidi ya ubaguzi. Hakuna taasisi yoyote ambayo imetengwa, ikiwa ni pamoja na polisi", amesema Rais Barack Obama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.