Pata taarifa kuu
MAREKANI-YEMEN-GUATANAMO

Habusu wa Yemen ahamishwa kutoka Guantanamo kwenda Italia

Serikali ya Marekani imemuhamishia Italia habusu wa Yemen kutoka jela la kijeshi la Guantanamo, Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema.

Jela la Guantanamo, lililo katika kambi ya jeshi la Marekani katika Kisiwa cha Cuba.
Jela la Guantanamo, lililo katika kambi ya jeshi la Marekani katika Kisiwa cha Cuba. Creative commons
Matangazo ya kibiashara

Fayiz Ahmad Yahia Suleiman, mwenye umri wa miaka 41 na alizaliwa nchini Saudi Arabia, alikua akifungwa bila mashitaka katika jela la Guantanamo kwa kipindi cha miaka14. Uamuzi wa kumhamisha ulitolewa mwaka 2010.

Baada ya zoezi hili, wafungwa 78 pekee ndio wanasalia katika jela la Guantanamo, ikiwa ni pamoja wafungwa 28 anao chukuliwa na utawala wa Obama kama ambao watahusika na zoezi hili la kuhamishiwa katika nchini za kigeni.

Washington imeishukuru Italia kwa "moyo wake wa kukubali kupokea raia huyo" na nia yake njema ya kuunga mkono juhudi za kulifunga gereza la Guantanmo, imeongeza Pentagon katika taarifa yake, ikibaini kwamba ina uhakika kuwa uhamisho huo unakubaliana na viwango vya kimataifa.

Utawala wa Obamaunatafu kupata, hadi mwisho wa muhula wa rais Barack Obama, mwezi Januari mwakani, nchi zitakazokukubali kuwapokea wafungwa ambao wanaruhusiwa kuhamishwa.

Wafungwa 50 ndio hawataachiliwa huru katika kambi hiyo ya wafungwa ambapo Barack Obama aliahidi kufunga jela wanakozuiliwa.

Miongoni mwa wafungwa 28 watakaohamishwa, 21 ni raia wa Yemen, jambo ambalo linausumbua utawala wa Marekani kwa sababu hautaki kuwarudisha katika nchi yao inayokabiliwa na machafuko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.