Pata taarifa kuu
MAREKANI-BARACK OBAMA-MAUAJI

Askari polisi 4 wauawa katika mkutano wa hadhara Dallas

Askari polisi wanne wameuawa na wengine saba wamejeruhiwa ikiwa ni pamoja na majeruhi wengi ambao wako katika hali mbaya baada ya kushambuliwa kwa risasi Alhamisi hii usiku na kundi la watu wenye silaha katika mji wa Dallas, nchini Marekani.

Maandamano dhidi ya ukatili wa polisi kwa watu weusi nchini Marekani, Dallas 7 Julai 2016.
Maandamano dhidi ya ukatili wa polisi kwa watu weusi nchini Marekani, Dallas 7 Julai 2016. Laura Buckman / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo linatokea baada ya raia wawili weusi kuawa na askari polisi siku mbili mfululizo mwanzoni mwa juma. Inaarifiwa kuwa shambulio hilo litokea wakati mamia kwa maefu ya raia walikua katika mkutano wa hadhara uliandaliwa kwa kupinga, baada ya mauaji ya watu wawili weusi waliouawa na vikosi vya usalama nchini Marekani.

"Usiku wa leo, inaonekana kwamba watu wenye silaha waliwashambulia kwa risasi askari polisi 10 kutoka ngome wakati wa maandamano (...) askari polisi watatu walifariki papo hapo, wawili wanafanyiwa upasuaji na watatu wako katika hali mbaya," David Brown, mkuu wa polisi katika mji wa Dallas amesema, katika taarifa yake. Na kuongeza kuwa maafisa wengine wawili walipata majeraha madogo.

Visa vya mauaji vimekithiri nchini Marekani tangu mwanzoni mwa juma hili, ambapo Wamarekani Weusi wawili waliuawa kwa kipindi cha siku mbili mfululizo.

Itafahamika kwamba askari polisi Weupe wamekua wakinyooshewa kidole cha lawama kuhusika katika visa mbalimbali vya mauaji ya watu Weusi nchini humo.

Rais Obama wa Marekani Barack Obama alisema Alhamisi usiku kuwa mauaji ya kikatili ya watu wawili weusi raia wa Marekani yaliyofanywa na polisi kama mengine yaliyotokea ni jambo kila Mmarekani ambaye anapaswa kulichukia.Rais Obama amesema ubaguzi umesababisha imani ya jamii kupungua dhidi ya polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.