Pata taarifa kuu
MAREKANI - OBAMA

Obama awabeza wabunge wa Republican

Rais wa Marekani Barack Obama amelitaka Bunge la Congress lenye wabunge wengi wa Chama cha Republican kupitisha sheria ya kudhibiti uuzwaji silaha kiholela ili kukabiliana na mauaji ya kigaidi nchini humo.

Rais wa Marekani, Barack Obama akihutubia familia za watu 49 waliouawa. Kulia kwake ni makamu wa rais Joe Biden
Rais wa Marekani, Barack Obama akihutubia familia za watu 49 waliouawa. Kulia kwake ni makamu wa rais Joe Biden REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Barack Obama ametoa kauli hiyo mjini Orlando ambako alikutana na familia za watu 49 waliouawa katika klabu moja ya usiku na kuongeza kuwa Marekani inapaswa kupitia upya sheria ya umiliki wa silaha.

Rais Obama wa Chama cha Democrat ameeleza kuumizwa kwake kutokana na tukio hilo na kueleza kuwa umefika wakati kuibua mjadala mpya juu ya umiliki wa silaha ili hatimaye kudhibiti silaha ambazo zimekuwa zikitumika kutekeleza mashambulizi na mauaji.

Rais wa Marekani, Barack Obama akiwa na makamu wake, Joe Biden, wakiweka shada la maua ikiwa ni ishara ya kuomboleza vifo vya watu 49 waliouawa kwa kupigwa risasi, 16 june 2016 Orlando.
Rais wa Marekani, Barack Obama akiwa na makamu wake, Joe Biden, wakiweka shada la maua ikiwa ni ishara ya kuomboleza vifo vya watu 49 waliouawa kwa kupigwa risasi, 16 june 2016 Orlando. REUTERS/Carlos Barria

Rais Obama amesema kwa wabunge wanaopinga kupitishwa kwa sheria ya udhibiti wa silaha, wanapaswa kujibu maswali ya familia za wahanga waliouawa kwenye mashambulizi ya kigaidi.

Akiwa mwenye huzuni alipohudhuria mazishi ya kwanza ya watu waliouawa kwenye shambulio la juma hili, rais Obama ameeleza nia yake ya dhati ya kutaka kuona sheria hii inapitishwa hata kabla hajamaliza muhula wake.

Bunge la Congress limekuwa likipinga kutungwa kwa sheria mpya ya umiliki wa silaha kwa madai kuwa hatua hiyo itakuwa inavunja katiba ya nchi kuhusu uhuru wa kumiliki silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.