Pata taarifa kuu
MAREKANI-CUBA-USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Havana yajiandaa kwa ziara ya kihistoria ya Barack Obama

Kwa mara ya kwanza baada ya miaka 88, rais wa Marekani atafanya ziara rasmi nchini Cuba. Ziara ambayo haikua inafikiriwa bado kwa mwaka mmoja kabla ya nchi hizo mbili kutangaza kufufua mahusiano yao ya kidiplomasia.

Watalii wakipita nyuma ya bango linaloadhimisha ujio wa Barack Obama. Havana, Machi 18 2016.
Watalii wakipita nyuma ya bango linaloadhimisha ujio wa Barack Obama. Havana, Machi 18 2016. AFP PHOTO/YAMIL LAGE
Matangazo ya kibiashara

Barack Obama anawasili Jumapili hii katika mji mkuu wa Cuba, Havana, ambapo atakuepo hadi Jumanne ijayo, akiwa na mkewe na mabinti zake wawili, uthibitisho kwamba anaipa umuhimu mkubwaziara hii. Ziara ambayo imesubiriwa kwa hamu na gamu nchini Cuba ambapo mamlaka wameweka uwezo wa kutosha wa kumpokea rais ambaye atabaki katika historia ya nchi hiyo.

Kamwe mamlaka ya Cuba haijawahio kuweka uwezo mkubwa kwa ziara ya rais yeyote anayeitembelea nchini hiyo. Ujio wa Barack Obama, unasubiriwa jioni Jumapili hii kwa ziara ya kihistoria na ambaye ataanza ziara yake rasmi kesho, Jumatatu.

Raia wa Cuba wanaonekana na furaha kubwa ya kumuona rais wa Marekani, amabaye anaitembelea nchi hiyo baada ya miaka 88, kufuatia kuvunjika kwa uhusiano kati ya Marekani na Cuba.

Waletwa kwa gari

Lakini kazi, zikisalia saa chachekabla ya kuwasili kwa rais wa Marekani, bado hazikamilika. Wafanyakazi wanaendelea kuweka lami kwenye barabara zilioharibika, pia wanakarabati taa za barabarani na hasa kamera za ulinzi.

"Kutokana na hatua ya mtazamo wa hatua za usalama, kila kitu kimewekwa sawa, amehakikisha mkazi wa mji wa Havane, Dieguez. Pia miundombinu. Shughuli pia zimeendeshwa katika maeneo ambapo [Barack Obama] anatakiwa kupita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.