Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA

Marekani: Marco Rubio asitisha mbio za urais

Marco Rubio mmoja wa wagombea wa chama cha Republican anayesaka tiketi ya kuwania urais kupitia chama hicho amejitoa katika mbio hizo. Seneta huyo wa Florida amechukua uamuzi huo baada ya kushindwa nyumbani katika mchujo wa chama hicho.

Seneta kijana Marco Rubio ajiondoa katika mbio za kusaka tiketi ya kuwania urais kupitia chama cha Republican.
Seneta kijana Marco Rubio ajiondoa katika mbio za kusaka tiketi ya kuwania urais kupitia chama cha Republican. REUTERS/Dave Kaup
Matangazo ya kibiashara

Jumanne hii usiku Marco Rubio alisitisha kampeni yake ya kuwania urais kupitia chama chake cha Republican.

Donald Trump, mgombea anayepewa nafasi kubwa ya kushinda katika chama hicho amekaribisha uamuzi wa mshindani wake Marco Rubio, licha ya kumshambulia kwa maeneno makali hivi karibuni.

Akiuhutubia umati wa wafuasi wake katika hoteli ya Mar-a-Lago, Trump amesema Rubio ni mgombea “mkali, mwerevu” na mwenye matumaini makubwa siku za usoni.

Donald Trump, ambaye anaongoza katika chama cha Republican, amejinyakulia ushindi mwengine katika kura za mchuzo za Jumanne hii ambapo Hillary Clinton ameongeza kupata ushindi kupitia chama cha Democratic.

Ushindi wa bilionea huyo, mwenye umri wa miaka 69 katika jimbo la Florida umetamatisha mbio za Seneta kijana Marco Rubio, ambaye si hatoshikilia bendera ya chama cha Republican katika uchaguzi wa urais wa Novemba 8.

Donald Trumpa kutoka New York ameshinda katika majimbo matatu ambayo ni pamoja na North Carolina, Illinois na Florida katika katika kura za mchujo wa chama cha Republican Jumanne hii.

Ted Cruz, hajashinda jimbo lolote kati ya majimbo matano yaliyoshiriki mchujo huo.

John Kasich amepata ushindi katika jimbo lake la Ohio, ikiwa ndio ushindi wake wa kwanza kabisa tangu zoezi hilo kuanza.

Hillary ashinda katika jimbo la Ohio

Usiku wa Jumanne ulikua mzuri kwa Hillary Clinton, ambaye baada ya kushindwa mwaka 2008 katika kura za mchujo za kusaka tiketi kuwania urais kupitia chama cha Democratic na Barack Obama, mgombea huyo anayeongoza katika chama hicho ana matumaini wakati huu kuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya Marekani kufikia Ikulu ya Marekani.

Mbali na Florida, waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani pia ameshinda katika jimbo la North Carolina dhidi ya seneta Vermont Bernie Sanders.

Lakini ushindi wake mkubwa wa Jumanne jioni ni ule wa Ohio, jimbo lenye viwanda vingi ambapo mshindani wake amepata nafasi nzuri.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.