Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA

Wamarekani wapiga kura za mchujo za "Jumanne Kuu"

Wamarekani wameanza kupiga kura za mchujo za "Jumanne Kuu," hatua ya mbio katika mashindano ya kushikilia Ikulu ya White House wakati ambapo Donald Trump na Hillary Clinton wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda katika kura hizo wana imani ya kuwashinda wapinzani wao katika majimbo kadhaa.

Wapiga kura wakijiandaa kupiga kura katika uwanja wa mazoezi mjini Atlanta (Georgia), Machi 1, 2016.
Wapiga kura wakijiandaa kupiga kura katika uwanja wa mazoezi mjini Atlanta (Georgia), Machi 1, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Zoezi hili la kupiga kura limeanza katika majimbo kumi ambapo vyama vya Democratic na Republican vinawafuasi wengi, na litaendelea katika jimbo la Colorado ambapo wafuasi wa chama cha Democratic wanaendelea piga kura, kabla ya kuhitimisha na mjadala wachama cha Republican katika jimbo la Alaska.

mfanyabiashara Donald Trump ana matumaini ya kupata ushindi mkubwa mbele ya washindani wake wanne wa chama cha Republican wakati ambapo Hillary Clinton anakabiliana na Seneta Vermont Bernie Sanders, hasa katika majimbo ya kusini ambapo watu wachache wana imani ya kumpigia kura.

"Siyo rahisi kuwa na shauku kwa mtu ambaye yuko katika kazi za umma kwa muda mrefu, lakini nadhani Hillary Clinton ataifanya vizurinchi yetu ikiwa ataibuka mshindi," amesema Rusty,ambaye aliku kupiga kura katika mji wa Alexandria, katika jimbo la Virginia.

Katika mji jirani wa Arlington, kulikuwa na motisha mapema asubuhi na mpiga kura mmoja ameeleza: ". Kwa kawaida ntkipigia kura chama cha Democratic, lakini Trump ananitia wasiwasi "

"Mimi sijui nini la kufanya," ameendelea, na kupendekeza kwamba anaweza wakati huu kushiriki katika kura za mchujo wa chama cha Republican ili kujaribu kumzuia bilionea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.