Pata taarifa kuu
ARGENTINA-AJALI-USALAMA

Argentina: zaidi ya askari polisi 40 wamefariki katika ajali ya basi

Zaidi ya askari polisi arobaini wamefariki katika ajali ya basi lililokuwa likiwasafirisha, kaskazini magharibi mwa Argentina, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa Jumatatu na viongozi wa nchi hiyo.

Mtazamo wa angani ukionyesha basi lililofanya ajali karibu na mji wa Salta Desemba 14, 2015.
Mtazamo wa angani ukionyesha basi lililofanya ajali karibu na mji wa Salta Desemba 14, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Askari pilisi 41 wamefariki na kuna askari polisi kumi ambao wamelazwa hospiali, ikiwa ni pamoja na wanne ambao wako katika hali mbaya", amesema Francisco Marinaro, mkurugenzi wa usalama wa umma katika mkoa wa Salta, eneo lenye milima ambako ajali hiyo ilitokea .

Basi lililokuwa limewasafirisha askari polisi liliacha barabara na kuanguka kwa mita 15 kutoka kwenye daraja, usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu wiki hii.

Mapema Jumatatu hii alfajiri waokoaji waligundua mara ya kwanza miili 20 karibu na mto. Na kisha waliokoa miili mingine iliyonasa katika gari.

Basi hilo, ambalo lilikuwa ni sehemu ya msafara wa magari matatu ya polisi lilipinduka katika eneo lililokuwa patupu wakati dereva alijisahau baada ya kuelekea kwenye daraja, polisi imesema katika taarifa yake. Kwa mujibu wa mkuu wa usalama wa raia, ajali hiyo ilisababishwa na kupasuka kwa tairi.

"Wengi walikuwa askari polisi vijana", amesema Gustavo Solis, Meya wa mji wa Rosario de la Frontera, mji ulio karibu na eneo la ajali. Kwa mujibu wa kiongozi huyo, ajali hiyo ilitokea kwenye barabara mbovu. "Wale ambao wanajua eneo hilo vizuri huwa wakijaribu kuendesha gari wakati wa usiku", Gustavo Solis amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.