Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAUAJI-USALAMA

Marekani: mauaji ya San Bernardino yashukiwa kuwa ya kigaidi

Viongozi wa Marekani wanaendelea na uchunguzi kujua kwamba kuna kigaidi ili kueleza kile kilichosababisha wanandoa wenye asili ya Pakistan kuua watu 14 Jumatano katika jimbo la California, mauaji mabaya kuwahi kutokea nchini Marekani.

Wachunguzi  wa Marekani wanasema kuwa kuna uwezekano mauaji ya San Bernardino yana uhusiano na ugaidi.
Wachunguzi wa Marekani wanasema kuwa kuna uwezekano mauaji ya San Bernardino yana uhusiano na ugaidi. REUTERS/Mike Blake
Matangazo ya kibiashara

Lakini wachunguzi hawana ushahidi kwamba Farook alikua hasa amejiunga na kundi la kigaidi.

Viongozi wa jimbo la California walitangaza Alhamisi watu 14, wenye umri wa miaka kati ya 26 na 60, waliouawa kwa risasi katika mji wa San Bernardino Jumatano wiki hii na mfanyakazi mwenzao, Syed Farook Malik na mkewe Tashfeen.

Aurora Godoy, mwenye umri wa miaka 26, raia wa San Jacinto, katika jimbo la California (Magharibi mwa Marekani), alikuwa kijana mdogo, na Isaac Amanios, mwenye umri wa miaka 60, aliyekua na umri mkubwa kuliko wote miongoni mwa wanawake sita na wanaume nane ambao walipoteza maisha katika mauaji mabaya kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka mitatu nchini Marekani.

Wengi mwa watu waliouawa ni kutoka miji midogo katika jimbo la California, lakini Shannon Johnson, mwenye umri wa miaka 45, ni kutoka Los Angeles, mji wa pili wa Marekani.

"Mauaji haya ni janga kubwa la kibinafsi kwa familia, marafiki, wafanyakazi wenza wa waathirika na watu ambao walikuwa sehemu ya maafisa wa Idara za huduma za dharura," Mkuu wa mji wa San Bernardino, John McMahon, amesema katika taarifa yake.

Watu 21 pia walijeruhiwa, baadhi walikua bado katika hali mbaya Alhamisi wiki hii wakati wauaji walipowashambulia watu kwa risasi katika chakula cha mchana cha Krismasi kwa wafanyakazi wa Idara ya Afya katika mji wa San Bernardino, ambapo Syed Farook aliajiriwa kama mkaguzi wa afya katika mgahawa ulioshambuliwa.

Polisi iliendesha msako nymbani kwa Syed Farook Malik na kukuta bunduki nyingi za kivita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.