Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-UFISADI

FIFA: wanane miongoni mwa watuhumiwa 16 wakiri kosa la ulaji rushwa

Vyombo vya sheria vya Marekani vinataka kuendelea harakati zake kubwa katika Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA), ambapo rushwa imekithiri kwa mujibu wa vyombo hivyo.

Waziri wa Sheria wa Marekani Loretta Lynch katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu kashfa ya rushwa kwenye FIFA, Desemba 3, 2015 Washington.
Waziri wa Sheria wa Marekani Loretta Lynch katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu kashfa ya rushwa kwenye FIFA, Desemba 3, 2015 Washington. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wapya kumi na sita, wote kutoka Amerika ya Kati na Kusini, wameshtakiwa Alhamisi wiki hii, ikiwa ni pamoja na manaibu rais wawili waliokamatwa alfajiri katika mji wa Zurich.

"Kwa kila mmoja wa maafisa wenye hatia ambao mumebaki mkijificha, na kuwa na matumaini kuwa hamtofichuliwa na uchunguzi unaoendelea, tambuweni kwamba hamtofika popote na hamtokwepa sakata yetu", Waziri wa sheria wa Marekani, Loretta Lynch, ametishia katika mkutano na waandishi wa habarii mjini Washington.

"Kila mmoja wa watuhumiwa wapya 16 anakabiliwa na kosa la rushwa iliyopangwa na makosa mengine yanayohusiana na ukiukwaji uliofanywa katika utekelezaji wa majukumu yake", Lynch ameongeza. Kwa mujibu wa waziri huyo wa sheria, "kiwango cha usaliti wa imani katika kesi hii kinatisha na kiwango cha rushwa ni jambo lisilokubalika."

Mwishoni mwa mwezi Mei, mahakama ya Marekani iliwachunguza watu 14 (ikiwa ni pamoja na maafisa tisa wajumbe wa sasa au wa zamani wa FIFA).

Watuhumiwa wanane wamekiri kuhusika kwao katika mfumo wa rushwa katika Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA) . Kwa mujibu wa Bi Lynch, kashfa ya rushwa ambayo ilisambazwa katika Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA) ni kiasi ya Dola milioni 200 tangu mwaka 1991.

"Watuhumiwa wanane wamekubali kosa kwa ushiriki wao katika mfumo wa rushwatulioweka wazi", amesema waziri Lynch, akiongeza kuwa watano kati yao hawakua katika mfululizo wa kwanza wa mashtaka ulioanzishwa na viongozi wa Marekani miezi sita iliyopita.

Viongozi wa CONMEBOL wanaoshatakiwa Marekani: Juan Ángel Napout; Manuel Burga; Carlos Chavez; Luis Chiriboga; nembo; Marco Polo del Nero; Eduardo Deluca; José Luis Meiszner; Romer Osuna; Ricardo Teixeira.
Viongozi wa CONMEBOL wanaoshatakiwa Marekani: Juan Ángel Napout; Manuel Burga; Carlos Chavez; Luis Chiriboga; nembo; Marco Polo del Nero; Eduardo Deluca; José Luis Meiszner; Romer Osuna; Ricardo Teixeira. NICHOLAS KAMM/AFP

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.