Pata taarifa kuu
RAEL-MAREKANI-USHIRIKIANO

US-Israel: Netanyahu asubiriwa mjini Washington kujadili ulinzi

Wakati ambapo vurugu zikiendelea katika Mashariki ya Kati, Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, atakutana Jumatatu hh, Novemba 9 mjini Washington na Rais wa Marekani Barack Obama.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akisisitiza jambo alipokuwa na mazungumzo na rais wa Marekani Barack Obama
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akisisitiza jambo alipokuwa na mazungumzo na rais wa Marekani Barack Obama Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mkutano wa kwanza wa ana kwa ana tangua mwaka uliopita na tangu kufanyike makubaliano ya nyuklia ya Iran. Uhusiano kati ya wawili hawa umeendelea kudorora, lakini licha ya tofauti zao, viongozi hawa wawili wana masuala mengi ya kujadili pamoja, ikiwa ni pamoja na suala la Iran, Syria, kuzuka upya kwa vurugu kati ya Wapalestina na Israel, na Mkataba ujao ulinzi kati ya Washington na Tel Aviv.

" Mkutano huo na Obama ni muhimu kwa muendelezo wa misaada ya Marekani kwa Israel ", amesema Waziri mkuu wa Israel kabla ya ziara yake Washington. Katika mwaka 2017 kutaanzishwa mpango wa msaada wa kijeshi kwa kipindi cha miaka 10 na Benjamin Netanyahu anaweza kuomba kuongezwa kwa kiwango hicho ikilinganishwa na dola bilioni 3 ambazo Israeli inapata kila mwaka kutoka kwa mshirika wake Marekani.

Hoja kuu ya Israel ni kujilinda dhidi ya tishio la Iran, baada ya mpango wa nyuklia kufikiwa mwezi Julai kati ya Tehran na nchi zenye nguvu, ikiwa ni pamoja na Marekani, amearifu mwandishi wetu mjini Jerusalem, Murielle Paradon.

Makubaliano yalielezwa na Benjamin Netanyahu kama "makosa ya kihistoria". Lakini "faili ya nyuklia ya Iran imefungwa ", maafisa walio karibu Barack Obama wamesema.

Suala ambalo bado linatia wasiwasi, hata hivyo, ni Tehran kuendelea kusaidia baadhi ya makundi ya kigaidi. Ikulu ya White House inatambua hilo. Mazungumzo juu ya kuanzishwa upya msaada wa jeshi la Marekani kwa Israel yatapewa kipao mbele katika mkutano wa viongozi hao wawili, amearifu mwandishi jijini Washington, Anne-Marie Capomaccio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.