Pata taarifa kuu
MAREKANI-SYRIA-URUSI-USHIRIKIANO

Marekani yalaani ziara ya Assad Moscow

Marekani imeshtumu vikali hatua ya Urusi kumkaribisha Rais wa Syria Bashar Al Assad jijini Moscow.

Bashar Al Assad, rais wa Syria, akizungumza na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wakati wa mkutano mjini Moscow tarehe 20 octobre.
Bashar Al Assad, rais wa Syria, akizungumza na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wakati wa mkutano mjini Moscow tarehe 20 octobre. REUTERS/Alexei Druzhinin/RI
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya White House imesema inashangazwa na hatua ya Urusi kumkaribisha raiso huyo wa Syrai ambaye ametekeleza mauahi ya raia wake kwa kutumia silaha za kemikali.

Rais Assad alizuru Urusi siku ya Jumanne, na kukutana na rais Vladimr Putin wiki tatu tu baada ya Moscow kuanza kutekeleza mashambulizi ya anga katika ngome za Islamic State na waasi wanaompinga Assad.

Akiwa nchini Urusi, Rais Assad alimshukuru sana Rais Putin kwa kutekeleza mashambulizi hayo ambayo anasema yamesaidia kukabiliana na Islami State na kuzuia kundi hilo kusambaa katika maeneo mengine.

Marekani imeendelea kutofautiana na mashambulizi haya ya Urusi na kuyashtumu kwa kuwalenga waasi wanaomtaka Rais Assad kuondoka madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.