Pata taarifa kuu
MAREKANI-PAPA-USHIRIKANO-DINI

Papa Francis atamatisha ziara yake Marekani

Papa Francis ametamatisha ziara yake nchini Marekani Jumapili hii iliyopita baada ya kuadhimisha Misa kubwa katika mji wa Philadelphia, kituo cha mwisho cha ziara ya siku sita wakati ambapo aliagiza ujumbe wake juu ya masuala tata kama vile uhamiaji, mazingira au familia.

Mtaa wa Benjamin Franklin wakati wa Misa ya Papa Francis katika mji wa Philadelphia, Septemba 27, 2015.
Mtaa wa Benjamin Franklin wakati wa Misa ya Papa Francis katika mji wa Philadelphia, Septemba 27, 2015. JEWEL SAMAD/AFP
Matangazo ya kibiashara

" Sijawahi kuona shauku kam hii, sote ni wamoja ", amesema akishangaa Manuel Portillo, mkazi wa Guatemala, mwenye umri wa miaka 54, ambaye anaishi katika mji wa Philadelphia kwa miaka 22 na amekaribisha maneno ya "ajabu" ya Papa kuhusu uhamiaji.

Ilikuwa ziara ya kwanza ya Jorge Bergoglio, mwenye umri wa miaka 78, katika nchi ya Marekani, ambayo ilimpeleka hadi Washington, kisha New York na Philadelphia, ambako ambapo alitamatisha mkutano wa 8 wa dunia wa familia za waumini wa Kanisa Katoliki. Mkutano mwengine umepangwa kufanyika katika miaka mitatu ijayo mjini Dublin.

Mbele ya zaidi ya watu milioni 1, kwa mujibu wa Vatican, Papa francis alisherehekea Misa kubwa ya mwisho baada ya kukutana asubuhi na waathirika wa kingono na wafungwa.

Wakati Misa hiyo, Papa alirejelea mambo mawili ambayo tayari ameyaongelea katika hotuba yake kwa Bunge na Umoja wa Mataifa: ulinzi wa familia ambao amesisitiza kuanzishwa pamoja na ulinzi wa mazingira.

Papa Francis kwa muda wa nusu saa aliwapokea wanawake watatu na wanaume wawili, waathirika wa vitendo vya ngono viliyotendwa sio tu na makasisi bali pia na walezi au jamaa wa familia zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.